Search

Pastor Imani Oscar Katana

GREETNGS FROM LIWALE-SOUTHERN TANZANA

Dear friends salute you in JESUS name.

I glorify GOD almight for such a wonderful opportunity to minister the Word of GOD to the church of southern part in Liwale -Lindi region. The whole week sense 28/3/-4 /4/2021.

The Holyghost is setitng free people from bondage.

The presence of GOD overshadow us every service.

Be blessed

AJALI ZA KUJALI

Haleluya! Atukuzwe MUNGU juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.Mpendwa msomaji wangu ni jumapili nyingine tena tunakutana kwenye madhabahu hii ya kona  ya Moto ulao.Ambapo kwa nitakuletea mfululizo wa somo hili la ajali za kujali.Karibu ufuatane nami

Kujal ni jambo zuri ambalo miziz yake ni upendo, katika sifa za upendo kama zilivyoorodheshwa kwenye Wakorintho wa 13 unaona , neno kujali likiwa halijaandikwa hapo moja kwa moja lakini unaweza kuona matendo kama upendo hufadhili , upendo haungalii mambo yake wenyewe,ukitazama kwa ukaribu maneno haya utagundua kwamba yeyote mwenye upendo ni atauwa n mtu anayejali.Kujali ni hali ya kutoa mwitikio chanya katika matukio ya wengine.Mtu anayejali n mwenye kuwahurumia wengine.

Kujali ni tabia ya waungwana watu wacha MUNGU, katika biblia Luka18:2-6  yuko mtu mmoja ambaye alijipambanua wamba  hamchi MUNGU wala hajali watu.Mbingu zikamtambua kama kadhi dhalimu nakuambia ukweli kwamba mtu yeyote unayejinasibu kwamba hujali hutaacha kutambuliwa kama mtu uliyedhalimu.Unajitutumua kwa kizungu kwamba ” I don’t care” hii sio sahihi unapaswa kuwa mtu unayejali.

Ziko ajali mbalimbali zinazoawapata watu wanaojali kiasi kwamba wanajuta kwa kujali kwao na kudhamlilia peupe au kwa siri kuacha kujali watu.Katika makala hii nitakuwa nikieleza ajali zinazowatoea weng wanaojali na namna unavyoweza kukabiliana nazo bila kuacha kujali. Nmeziita ajali kwa sababu huwa zinawatokea watu bila kutarajia  ,kila msafirii anatarajia kufika salama kule anakowenda.Lakini ajali inavyotokea huharibu matarajio ya msafiri. Kila msafiri katika barabara ya kujali  huwa anataka kuona kwamba anafikia mwisho mwema wa kujali kwake ,badala yake hujikuta akitendewa vinginevyo kwa namna yenye kumuumiza.

Wanasema kujali sio kazi  kumpata mtu wa kukujali.Wako wengi wanaojiuta wamepata ajali hii ya kujali hususani wazazi wanaowekeza kwa watoto wao.Wakidhani kwamba  watakusanywa na kujalwa katika uzee wao jambo ambalo unakuta halifanyiki. Niliwahi kusoma andiko mmoja kwamba wazazi wawili wanawajali na kuwalea watoto kum na wakakua na wakafanikiwa  lakini watoto kumi wanashindwa kuwalea na kuwajali wazaz wawili. Mpendwa msomaji wangu nakukumbusha kusimama na kuwa mtu unayejali wazazi.

Wazaliwa wa kwanza katika familia pia ni wahanga wa ajali za kujali unaweza kuona jinsi wanavyojitoa kuwajali wadogo zao. Wakijikamua wa jasho   damu kusomesha , uwasadia wadogo zao kwa hali na mali lakini punde wadogo zao hao wanapofanikiwa huwa hawana muda wa kurejesha fadhili hizo.Ooooh wakaka na wadada ambao mmejikuta kwenye hii ajali nataka kuwafunga na kuwapaka  divai jeraha zenu imeandikwa kwa kitabu cha Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.Hey nafurahia andiko hili kwamba apandacho mtu sio apanadapo  mtu , kwa hiyo usiogope hutavuna ulipopanda bali utavuna ulichopanda .Nakuombea wewe mzaliwa wa kwanza MUNGU akunulie watu watakaojali kama ulivyojali wao.

Kwa namna hii wako watu wengi wamejikuta hawana muda wa kujal tena kwa vile tu wamejeruhiwa na watu waliowajali sana .Biblia anasema Marko 16:18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.Unaona hicho kipengele cha kunywa vitu vya kufisha usidhani kwamba ni vinywaji vya kawaida hasha!

MAMBO KUMI YA KUFANYA ILI UWEZE KUPATA KIBALI MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU

SEHEMU YA 1

 MAMBO KUMI YA KUFANYA ILI UWEZE KUPATA KIBALI MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU.

MAHUBIRI YA JUMAPILI  07/03/2021

NA: MCHUNGAJI IMANI OSCAR KATANA.

Mpendwa wangu ninakusalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI  aliyehai .Karibu katika ujumbe wa leo ambao Roho mtakatifu imempendeza tuweze kujifunza kwa habari ya kibali.Kibali ni ile hali ya kukubaliwa ,kupendwa na kupendelewa ,kufurahiwa na kupewa chochote unachokihtaji.Miongoni mwa vitu muhimu vnavyoweza kufanya Maisha yako yawe mazuri hapa dunian I basi n Maisha yenye kibali .MUNGU wetu atufundshaye ili tupate faida anatufundisha siku ya leo ili kwa somo hili ikaweko faida katika Jina la YESU.

Yafuatayo ni mambo kumi ya kufanya ili uweze kupata kibali mbele za MUNGU   na wanadamu;

1:KUTENDA MEMA

Matendo mema huleta kibali MUNGU alipokuwa anaona wivu kwa ajili ya  ndugu yake Habili . Mwanzo 4:7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

Mpendwa wangu tenda mema utapata kibali.Fanya mema kuliko wenine nawe utaona kibali chako kikiongezeka . Pokea uwezo huo wa kutenda mema kwa uweza wa jina la YESU.

2:KUSHIKA  NENO LA MUNGU.

Katika mithali Sura 3 unaona mambo makuu mawili ili uweze kupata  KIBALI NA AKILI NZURI. Mungu wetu anayo hazina ya Kibali na akili nzuri kwa  watu watakaolishika  na wale  watakaotembea katika rehema na kweli.

Mithali 3:1-4

1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.

 2.Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.

 3 Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

 4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu

Neno Rehema limetafsiriwa kwa lugha ya kingereza kama huruma  ndio maana unakuta unapowauhurumia wengine uwe na uhakika kwamba utakuwa na kibali.Kinyume chake ni kweli kwa mtu  mkatili asiye na huruma watu huwa wanamuogopa na kuwa mbali naye.

3:KIBALI KUTOKANA NA  KUTUMIKI KUSUDI LA MUNGU .

weza kulitambua kusudi la kuumbwa kwako uwe na  uhakika kabisa kibali cha MUNGU kitaachiliwa kwako kuhakisha kwamba unalifanikisha. Kbali hiki kilikuwa juu ya MUSA Kutoka 11:3 Bwana akawapa watu hao kibali machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na mabalbali choni pa watu wake.

Ukisoma kwa utulivu kuanzia mstari wa pili utagundua kwamba MUNGU aliachilia kibali kwamba kila walichokihtaji kutoka kwa Wamisri wakaweza kupatiwa. Hiki ndicho kibali alichokipata Nehemia mbele ya mfalme na kuruhusiwa  kupewa vitu kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa Yerusalemu.

Mungu wetu ambaye hhabadiliki na akuachilie kibali hiki sawa na lile kusudi la kuumbwa kwako katika jina la Yesu.

4:KIBALI  HUJA KWA MAOMBI.

Kuna watu wanasema kibali hakiombwi lakini utamuona Esta na Wayahudi wakiomba kibali kwa MUNGU aweze kupata kibali mbele za Mfalme. Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.  Esta 4:16

UFANIKIWE NA KUWA MASHUHURI

Mara nyingi umekuwa ukimuomba MUNGU akufanikishe na kukubarikia lakini katika siku ya BWANA ya Leo twende hatua moja zaidi

Imeandikwa ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehem. Ruth 4:11d

Ninaamini kwa sehemu BWANA MUNGU amekufanikisha, lakini hukujua kwamba kuwa mashuhuri yaani kuwa maarufu ni sehemu ya baraka. Nikiwa kuhani niliyepakwa mafuta na Roho Mtakatifu nakutamkia baraka ya kufanikiwa kazi ya mikono yako na ukawe mashuhuri katika jina la Yesu.

Ukafanikiwe katika mtaa wako, wilaya na mkoa wako naam ukawe mashuhuri katika nchi yako na dunia nzima. Sawa na imani yako na maono neno hili likawe lako. Nasema usifanikiwe tu kwenye huo

Uongozi

Huduma

Biashara

Ajira

Kilimo

na kila ufanyalo

Bali ukafanikiwe na kuwa mashuhuri kwa familia,ukoo,kanisa,mtaa/kijiji ,wilaya, mkoa, Taifa na Dunia nzima. Nakuombea kufanikiwa na kuwa mashuhuri maishani mwako katika jina la Yesu. Kama umepokea na useme amina

PROSPER AND BECOME FAMOUS

Many times you have been praying to GOD to make you prosper and bless you but today let’s go one step further.It is written …and you do worthily in Ephrathah, and be famous in Bethlehem. Ruth 4: 11dI believe in to some extent the LORD GOD has made you successful, but you did not know that being famous means is part of the blessing. As an anointed man of GOD ,I declare the blessing of the labour of your hands and may you be famous in Jesus mighty name.Be successful in your neighborhood, district and region and be famous in your country and the world.According to your faith and vision this word should be yours.I say don’t just succeed in thatLeadershipServicesBusinessJobsAgricultureand everything you doBut be successful and be famous starting to your family, clan, church, neighborhood / village, district, region, nation and the whole world.I pray that you will prosper and be famous in your life in Jesus name. If you have received and say amen.

IMANI KATANA preachings: *FIVE IMPORTANT PRAYER POINTS AS YOU ARE CROSSING TO MARCH*

.Dear reader and friend, I salute you in the name of JESUS ​​and invite you to hear the Word of GOD this Sunday which has the power to deriver you and give you new hope as we finish the second month and join the third month of this year 2021.Open and read with me the book of Psalms chapter 20: 1-4 There I have been revealed five things which are my prayers for you and I desire the great GOD to enable you to be yours this year in the name of JESUS. Welcome and come with me1.

*MAY THE LORD HEAR YOU IN THE DAY OF TROUBLE* .Ps. 20: 1

Our life here on earth are full of all kinds of troubles . Jesus Himself spoke of the world in which we suffer. He sent his disciples out like sheep in the midst of wolves. Worse enough, in the time of trouble, you are left alone.The people whom you depend on when you go through your tribulation will not see them, the wise proverbs say that even your own shadow flees you in the dark.But today I bring you good news that the LORD will answer you in the time of your trouble. The Psalmist in Psalm 18: 6 and Psalm 118: 5 testify that in my distress I called upon the LORD and he heard me. Shout ameeeen.

2: *MAY THE NAME OF THE GOD OF JACOB DEFEND YOU*

many names that you were hoping to defend you, are the first ones that have failed you. I have seen people who were volunteering to work professionally to get the names of those companies uplifted but that was not the case. In the might name of Jesus every knee should bow, of things in heaven, and things in earth, and things under the earth; and every tongue should confess that Jesus Christ is Lord, to the glory of God the Father.And there is no other name under heaven given among men by which we must be saved (Acts 4:12)…… IT IS MY PRAYER THAT GOD OF ISRAEL DEFEND YOU IN THE NAME OF JESUS.

.3: *MAY THE LORD SEND YOU HELP FROM THE SANCTUARY*.

No self-sufficient person receives help. GOD has the help to lead His people and that person will be you in the name of JESUS. Receive the Lord’s help inKnow Him and serve HimBusinessIn your officeIn your marriageIn your economyI pray to GOD help and lifts you up from his sanctuary4:

*REMEMBER ALL YOUR OFFERINGS* .Ps 20: 3

May God remember all your offerings as He remembered the offerings of Cornelius in the book of Acts chapter 10. He sent an angel to tell him what to do with you GOD to send the Holy Spirit and reveal to you what you must do in his kingdom.RemembervYou Like Dorcas of Acts 9:36 where her sacrifices did not leave her to be buried but made Peter go to Resurrection.Whatever dies in your life GOD may resurrect and I pray to GOD to remember all your sacrifices. You who hate being told to offerings have no part in this feature.

5: *GOD GRANT YOU ACCORDING TO YOUR OWN HEART*

.Beloved, God knows the needs of the heart and He always fulfills it.And Jabez was more honorable than his brethren; and his mother called his name Jabez, saying, Because I bore him with sorrow. And Jabez called on the God of Israel, saying, Oh that thou wouldest bless me indeed, and enlarge my coast, and that thine hand might be with me, and that thou wouldest keep me from evil, that it may not grieve me! And God granted him that which he requestedGOD GIVE YOU ALL THAT YOU ASK FOR.Bless you so much for today’s worship and you can make your offering at this altar by sending M-PESA 0752 352 116.

I WISH YOU A BLESSING AS YOU START THE THIRD MONTH OF 2021

Pastor Imani Oscar Katana

WhatsApp +255 752 352 116

Email:katanaimani@gmail.com

www.imanioscar.wordpress.com

Dar es salaam Tanzania

KUWA SEHEMU YETU KATIKA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LETU.

UMETEMBELEA BLOG YETU SO KWA BAHATI MBAYA UNAOMBWA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA HAPA KIGAMBONI

WASILIANA NA MCHUNGAJI KATANA KWA NAMBA+255 752 352 116

EMAIL:katanaimani@gmail.com

MAMBO MATANO TUNAYOKUOMBEA YAWE YAKO MWEZI WA TATU.

MAHUBIRI YA JUMAPILI YA MWISHO WA MWEZI PILI 2021

NA:MCHUNGAJI IMANI OSCAR KATANA

WhatsApp +255 752 352 116

http://www.imanioscar.wordpress.com

Facebook:Ev.Imani Oscar Katana.

Mpendwa msomaji na Rafiki yangu ninakusalimu katika jina la YESU karibu na uweze kusikia Neno la MUNGU jumapili ya leo lenye uwezo wa kukunua na kukupa tumaini jipya tunapoumaliza mwezi wa pili nakungia mwezi wa tatu.

Fungua na usome pamoja nami kitabu cha Zaburi sura ya 20 :1-4  Hapo nimefunuliwa mambo matano ambayo ni maombi yangu kwa ajili yako  natamani MUNGU mkuu akuwezeshe yawe yako katika mwaka huu kwajina la YESU. Karibu ufuatane nami

1.BWANA AKUJIBU SIKU YA DHIKI.Zab 20:1

Maisha yetu hapa duniani hujawa  na dhiki za kila namna.Yesu mwenyewe alisema ulmwenguni tunayodhiki. Aliwatuma wanafunzi wake kama kondoo katikati ya mbwa  mwitu.Na kibaya Zaidi wakati wa dhiki ni ile kuachwa peke yako.

Watu uliowategemea wakati upitapo kwenye dhiki yako hutawaona, isitoshe wenye hekima husema hata kivuli chako mwenyewe hukukimbia wakati wa giza.

Lakini leo ninakuletea habari njema ya kwamba BWANA akujibu wakati wa dhiki yako.Mtunga Zabur katika Zaburi ya 18:6 na Zab 118:5 zinatoa ushuhuda ya kuwa katika shida yangu nalimwita BWANA naye akanisikia .Rafiki nakuombea hakika BWANA AKAKUJIBU WAKATI WA DHIKI YAKO. Sema ameeeen

2: JINA LA MUNGU WA YAKOBO LIKUINUE

Yako majina mengi ambayo umeweza kuyatarajia yakuinue ndio  kwanza yamekuangusha.Nimeona watu waliokuwa wakijtoa kufanya kazi kwa weledi ili majina ya hizo kampuni yawainue lakini haikuwa hivyo na ndiposa MUNGU akamkirimia YESU jina kubwa sawa  Wafilip 2:9-11Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Tena hakuna jina  jingne chini ya walilopewa wanadamu ltupasalo kuokolewa kwalo Matendo ya mitume  4:12.ACHANA  NA MAJINA YOTE YALIYOKUANGUSHA NAKUOMBEA UNAPOUKANYAGA MWEZ WA TATU NA KUENDELEA JINA LA MUNGU WA YAKOBO; MUNGU WA ISRAEL LIKUINUE JUU SANA KATIKAAA JINA LA YESU.

3:AKUPELEKEE MSAADA KUTOKA PATAKATIFU PAKE.

Hakuna mtu anayejiweza ambaye anapokea msaada.  MUNGU anao msaada wa kuwapelekea watu wake na mtu huyo akawe wewe katiika jina la YESU.pokea msaada wa BWANA katika

Kumjua na kumtumikia

Biashara

Ofisini kwako

Kwenye ndoa yako

Kwenye uchumi wako

Nakuombea MUNGU na akuinulie msaada  kutoka patakatifu pake

4:AZIKUMBUKE SADAKA ZAKO ZOTE.Zab 20:3

Mungu azikumbuke sadaka zako zote kama alivyozikumbuka sadaka za Kornelio katika kitabu cha Matendo ya mitume sura ya 10. Akamtuma malaika amueleze mambo yampasayo kutenda nawe MUNGU amtume  ROho mtakatifu na akufunulie yale yakupasayo kutenda katika ufalme wake.

Akukumbuke Kama Dorkas wa Matendo ya MITUME  9:36 ambapo sadaka zake hazikumuacha azikwe bali zikafanya Petro aende Kumfufua.

Chochote kinachokufa katika Maisha yako MUNGU na akafufue nakuombea MUNGU akumbuke sadaka zako zote. Wewe unayechukia kuambiwa kutoa sadaka huna fungu katika kipengele hiki.

5:MUNGU NA AKUJALIE KWA KADRI YA HAJA YA MOYO WAKO.

Mpendwa wangu haja za moyo MUNGU anazijua na huwa huzitimiz.NAKUOMBEA HAJA ZOTE ZA MOYO WAKO MUNGU AKAZJALIZE KAMA  ALVYOFANYA KWA YABESI 1NYKT 4:9-10.

Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.  Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba

MUNGU NA AKUJALE HAYO YOTE UNAYOYAOMBA.

Barikiwa sana kwa ibada ya leo na waweza kutoa sadaka yako kwenye madhabahu hii kwa kutuma namba M-PESA 0752 352 116.

NAKUTAKIA BARAKA UNAPOANZA  MWEZI WA TATU…

HAPPY BIRTHDAY MAMA MCHUNGAJI IMANI KATANA.

Mungu akujalie utele

Uishi miaka mingi

Create a free website or blog at WordPress.com.

Up ↑