Suprise ni neno la kiingereza linamaanisha kupewa au kupata kitu kipya kizuri ambacho haukutarajia kukipata. Yaani ni kitu kinachokushangaza na kukuacha umeduwaa kwa furaha. Sasa nataka niseme nawe kwa habari ya MUNGU WETU KUHUSIKA NA KUSUPRISE WATU. Katika BIBLIA wafuatao MUNGU aliwa suprise.

1: OBED -EDOM MGITI HAKUJUA WALA HAKUPANGA KWAMBA SANDUKU LA AGANO LINGEINGIA NA KUKAA NYUMBANI MWAKE. (1SAMWEL 6:9-12)

 Naye Daudi akamwogopa Bwana siku ile; akasema, Litanijiaje sanduku la Bwana?
  Basi Daudi hakutaka kulileta sanduku la Bwana kwake mjini mwa Daudi; ila Daudi akalihamisha nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti.
  Sanduku la Bwana akalitia katika nyumba ya Obed-edomu, Mgiti, muda wa miezi mitatu; naye Bwana akambarikia Obed-edomu, na nyumba yake yote.
 Kisha mfalme Daudi akaambiwa ya kwamba, Bwana ameibarikia nyumba ya Obed-edomu, na vitu vyote alivyo navyo kwa ajili ya sanduku la Mungu. Daudi akaenda, akalileta sanduku la Mungu, toka nyumba ya Obed-edomu mpaka mji wa Daudi, kwa shangwe.


Obed-edom akashangaa tu sanduku la Agano la MUNGU wa Israel linaingia nyumbani kwake hakujua wal hakutegemea lakini MUNGU ALIMSUPRISE, KAMA ALIVYOMSUPRISE OBED-EDOM KATIKA JINA LA YESU ACHA MUNGU AKAKUSUPRISE NA WEWE KATIKA MAISHA YAKO KATIKA JINA LA YESU,.

2: YUSUFU MWANA YAKOBO HAKUWAHI KUPIGA KAMPENI AWE WAZIRI MKUU WA MISRI (MWANZ0 41:41-44)

 Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.
 Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
 Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri.
 Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri

Aliingi Misri kama mtumwa wa ndani house boy, lakini MUNGU wa suprise alimshngaza Yusufu na akawa mkuu katika nchi yote ya Misri MUNGU akakushangaze nawe katika maisha yako, mambo mazuri ambayo hujawahi kuyawaza yakakutokee katika JINA LA YESU.

3:MARIAMU HAKUWAHI KUOMBA KUMZAA YESU

Kulikuwa na mabikira Wengi katika Israel lakini maandiko yanasema Mariam alipata Neema machoni pa MUNGU

  Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.

Mariamu alipata neema, KATIKA JINA LA YESU NEEMA YA MUNGU ikawa juu yako katika mwezi huu na akakushangaze.

4: ELISHA HAKUWA MWANA WA NABII LAKINI AKAWA NABII BAADA YA ELIYA

Ilikuwapo Desturi katika Israel ya manabii kuwalea wana wa manabii, lakini Elisha yeyen alikuwa mtumishhi tu wa ELIYA lakini MUNGU wakushangaza alimshangaza ni miongoni mwa manabii 

nasema yeye MUNGU wetu ni WAKUSHANGAZA

5:MUDA USINGETOSHA KUTAJA HABARI ZA DAUDI, MUSA ,SAUL NA MANABII WALIOSHANGAZWA NA MUNGU WA KUSHANGAZA

Musa akiwa machungani alioona kijiti kikiwaka moto, akashangaa akasema nitageuka niyaone maono haya ya ajabu, alipogeuka MUNGU akasema naye kutoka katika ule moto    kutoka 3.

Daudi hautarajiwa kuwa mfalme wa Israel kutokana na nafasi yake kuzaliwa LAKINI MUNGU 

WA KUSHANGAZA ALIMSHANGAZA NA KUMPAKA MAFUTA KUWA MFALME WA ISRAEL

NASEMA NA WEWE MUNGU ATAKUSHANGAZA KATIKA JINA LA YESU

VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA.

 

Advertisements