UJUMBE WANGU KUPITIA GAZET NYAKATI UK 14
Nawasalimu katika Jina kuu la YESU,siku hizi imekuwa kama matangazo ya biashara kila kona utasikia kanisa lile lipo kwenye mfungo wa siku 40.utasikia mchungaji wao akisema nipo kwenye mfungo wa siku 21 na moja. Wakristo wengi wanaona fahari kujitangaza kwamba wapo kwenye mfungo pengine kwa sababu wanawaiga wanaowaongoza wamesahau yale BWANA YESU aliyotuagiza katika injili ya
Mathayo 6:16-21
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
KRISTO YESU aliongea waziwazi kwamba mambo ya maombi ya kufunga ni siri, haipaswi kutangazwa kwa umma wote, kutangazwa redioni au kwenye magazeti.Mimi nasema huo ni ufarisayo ambao Yesu aliukataza.Unapata wapi ujasiri wa kujitangaza kwamba upo kwa mfungo wakati YESU alikataza waziwazi. Sikatai katika mazingira ya watu wa kanisa au kikundi cha maombi kukubaliana kufunga lakini sio kila mtu ajue kwamba kanisa Fulani linafunga au mtumishi Fulani wa MUNGU yupo kwenye mfungo sasa.
Wapendwa katika BWANA hebu tuwe watii na kuliheshimu NENO kama Samweli ambaye hakuacha neon lake MUNGU lianguke chini naye BWANA alikuwa pamoja naye. 1samwel 3:19 .TUKITAKA MUNGU AWE PAMOJA NASI KATIKA KUFUNGA KWETU NI LAZIMA TUHAKIKISHE HATULIACHI NENO LAKE NGUKE CHINI. Unapotangaza na kuwaambi watu kuwa umefunga wakati YESU aliaiza kufunga ni siri, unaweza kuona MUNGU hawezi kuwa nawe kwa sababu umeliacha NENO lake lidondoke chini.
Kwa mtumishi yeyote anayetangaza kwamba yeye amefunga au kanisa lake limefunga kimsingi anataka umaarufu kwamba aonekane ni wa kiroho zaidi na awavute wengi waende kwake kuombewa wakiamni kuwa anazo nguvu nyingi kutokana na kufunga kwake. Huu sio mpango wa MUNGU yeye hatagawana utukufu na mwanadamu. Sikieni maneno ya Mwinjilisti enyi kanisa la Tanzania na duniani kote kufunga kutabaki kuwa siri ili kuwe na thawabu mbele za MUNGU wetu, lakini kama unataka kupata utukufu kwa wanadamu basi endelea kujitangaza kwenye vyombo vya habari kwamba upo kwenye mfungo wa siku 40 au ukitaka sema siku 100.
Neon la MUNGU haliwezi kuchuja wala halitabadilika eti kwa sababu Ulaya na Marekani wanafanya hivyo, hii ni kona ya moto ulao.ULE MOTO ULAO UPITE NDANI MWETU NA KUTAFUNA VITABIA VYA KIFARISAYO NDANI MWETU ILI TUFUNGE SAWA NA YESU KRISTO ALIVYOTUAGIZA.
Advertisements