TUJIFUNZE KUKOMALIA MAMBO
Mpendwa rafiki yangu , ninakusalimu katika jina kuu la YESU leo nimekuwa na safari nzuri kutokea Dar hadi Masasi , tutakuwa hapa hadi jumapili kwa ajili huduma ya NENO la MUNGU Mkutano Pamoja na semina.

kama ilivyokawaida mkononi nilikuwa na kitabu chenye kichwa The 21 irrefutable Laws of leadership cha John C. Maxwell.
Nimeshangaa kusoma maisha ya TR yaani Theodore Roosevelt rais wa 26 wa marekani.

Huyu mtu juhudi zake katika kuongoza, zilimfanya ateuliwe na chama chake kugombea kama makamu wa rais mnamo mwaka 1900 alipokuwa anafanya kampeni alipigwa risasi kifuani, lakini hakuacha hotuba yake alihutubia kwa takribani saa nzima na risasi kifuani mwake, na baada ya hapo akapelekwa hospitali na wasaidizi wake kutibiwa.

Juhudi hizi zilifanikisha kuwa makamu wa rais na baadaye kuwa raisi wa 26 wa marekani.
TR anatajwa kuwa miongoni mwa marais watano bora wa marekani, katika uongozi wake ndipo marekani ilianza kuwa taifa kubwa duniani.
Sasa wewe rafiki yangu, unakata tamaa ukiguswa kidogo tu , wakati wenzako risasi za kifua haziwazuii kufikia malengo yao.  Usikubali kususa au kuacha kazi kwa sababu ya wanaokupinga, usiwe mtu wa kuwakimbia maadui na kuwaacha wafurahie, tujifunze kwa huyu shujaa risasi kifuani na hotuba ikaendeleaa.

ukisusa wenzio wanakula

marufuku kukata tamaa, songa mbele utimize ndoto yako.

Advertisements