Dunia inaenda kasi sana, na tabia za watu zinabadilika wengi wamelizwa machozi ya damu. Acha mimi nikuonye tu wewe unayeawaamni watu utadhhani malaika hebu fuatana nami…

Dada yangu  binti yangu , nakusihi kwa huruma zake MUNGU achana na tabia ya kumuamini mtu kupindukia eti kwa  sababu tu amekuahidi kukuoa. Eti kwa vile amesema atakuoa ndio unachukua pesa unampatia eti kwamba mzalishe pamoja mtakapooana biashara ziwe zinaendelea. Wengine wamezitumia pesa hizo kwenda kulipa mahali kwa mwanamke mwenzio. acha maji yafuate mkondo wake urafiki uwe urafiki na uchumba  uwe uchumba kamwe usiufanye uchumba ukawa ndoa.

Na hakuna laana mbaya kama kufanya ngono na mume wako mtarajiwa kabla ya ndoa maana ukifanya hivyo unakuwa sio kwamba umesaidia kujenga mahusiano kuelekea ndoa bali unakuwa umebomoa kwa asilimia hamsini.

Nakushauri mdogo wangu acha kuingia gharama kubwa, eti unamuandaa ili uje kumuoa, unatoa mamilioni ya shilingi kumsomeshea akiwa bado mpenzi, baadaye unakuwa umemkutanisha na mwenzi wake ambaye alikuwa hawezi kumpata bila mamilioni yako.

miradi yote na uwekezaji wa pesa nyingi, usifanyike katika hatua urafiki wala katika uchumba , nashauri ufanyike katika ndoa. TRUST BUT NOT TOO MUCH. ukipuuzia siku moja utanikumbuka!

Mh! pia usimwamini rafiki wa zamani kwani watu hubadili tabia kila leo, atakujia akisema nikopeshe pesa wewe utajua ndio yuleyule wa zamani lakini kumbe mwenzako amekuwa kiumbe kipya sio yule unayemfahamu anakuliza, unabaki na majuto!

mimi nkukumbusha tu rafiki yangu, Usimwamini kupindukia hata malaika  kwani shetani naye hujigeuza awe kama malaika wa nuru.

MUNGU peke yake ndiye wa kuaminiwa kwa kupindukia.

barikiwa sana!

ndugu yako katika KRISTO  Imani O.K

 

Advertisements