Mpendwa msomaji ninakusalimu katika jina kuu la YESU KRISTO , nashukuru kwa jinsi ambavyo umekuwa ukifuatilia kona hii ya moto ulao.Wiki iliyopita nilimalizia sehemu ya tano ya Makala yangu iliyokuwa na kichwa mambo matano yenye umuhimu kuliko pesa, leo nitaanza mfululizo mpya wa Makala hii ambayo tutakuwa tunajifunza kwa mifano. Imeandikwa wala pasipo mifano hakuwaambia neno lolote Mathayo 13:34. Karibu tujifunze kwa mifano

Kulitokea ukame wa kutisha Katika mbuga moja, wanyama wote wakahamaūüź≠¬†kutafuta ūüĆĪ¬†¬† malisho katika mbuga zingine, isipokuwa kobeūüźĘ,¬†na kobe hakuhama mapema kutoka na na mwendo wake wa polepole.Alitamani kama angekuwa na mabawa na yeye aruke akatafute chakula kama ndege lakini asiweze, akaendelea kumuomba MUNGU amsaidie katika janga hilo.

Mungu huwa anajibu maombi siku moja mwewe na mke wake Wakiwa wanaruka angani, walimwona kobe akiwa anapatashida kukimbia janga lile la ukame, wakaamua kumsaidia, wakamwambia kobe kwamba watamsaidia kumbeba,kobe akafurahia sana msaada ule , hivyo baba mwewe akashika fimbo  mdomoni upande mmoja na mama mwewe upande mwingine, kisha kobe kwa mdomo wake atashikilia katikati, wakamuonya kwamba watakapoanza kuruka kobe ashikilie kijiti kwa mdomo wake wala asijaribu kufumbua kinywa chake kwa namna yoyote ile.

kobe akashukuru sana na akaahidi kijitahidi, safari ikaanza, walipoanza tu kunyenyuka tu, watu wakaanza kumzomea NA kutukana na kupiga mbiu wakisema Leo likobe na jumba lake linapaa. Kobe akavumilia, kelele  zile zikazidi kObe akaamua kuwajibu akasema acheni ujinga, alipofunua kinywa tu akawa ameachia fimbo aliyokuwa ameishikilia kwa mdomo akaanza kudondoka na alipofika Chini akawa amepasuka na kufa,

mpendwa  wangu kobe akafa kwa sababu ya kushindwa kuvumilia maneno na kujizuia kushambuliwa akaamua kufumbua mdomo wake na kuachia fimbo ya uhai aliyokuwa anaishikilia kwa mdomo.Sio kila kitu unachoshambuliwa unapaswa kujibu , kwani unapojibu waweza kujitumbukiza katika matatizo makubwa yanayoweza kugharimu Maisha yako.

Imeandikwa 1 Peter 3:10 Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. Ipo thawabu kubwa katika kujizuia, kila mmmoja wetu lazima ajitahidi kujizuia na kunena tu pale wakati upasapo kunena .

Wenye hekima husema laiti samaki angejua kwamba kwenye chambo ya mvuvi kuna ndoana asingefungua mdomo wake, tatizo ni kwamba samaki huona chambo pekee hajui kuna ndoana. Ndiposa hula chambo na kujikuta kanaswa na kufanyika chakula cha mvuvi. Mimi nakushauri kila wakati  uombe macho ya rohoni ili kwamba uweze kuona chambo  na ndoana pia, na kwa kujua hilo hautafumbua kinywa chako na utakuwa salama.

Maneno sio mapanga na wala sio malungu kwamba ukikaaa kimya yatakuumiza au yatakufanya uvuje damu,tumia hekima kufumbua kinywa chako, kobe alipoteza uhai wake kwa sababu alishindwa kunyamaza alipokuwa akishambuliwa, wakati unaposhambuliwa unahitaji neema ya kunyamaza.Kaa kimya na useme tu katika wakati muafaka hii itakufanya uione siku njema.

Ndugu yangu, katika maisha unatakiwa Kuwa mvumilivu sio kila jambo unatakiwa kujibu wakati mwingine unapojibu ndio unasababisha madhara Zaidi kuliko kukaa kimya, kumbuka hata kukaa kimya nako ni jibu,jitahidi kuwa makini pale unapofumbua kinywa chako ili usije ukajikuta unadondoka chini na kupasuka kama kobe.

Mungu ni wa huruma, huenda amakufanya usome Makala hii kwa sababu ya mambo yanayokujia mbele zako tumia akili, kamawe fahamu kwamba mdomo umeshikilia mti wa msalaba, usikubali kuachia msalaba kwa sababu ya hasira, wako wanaokuchokonoa tu ili wasikie sauti yako ukiwajibu halafu waitumie kukoroga mambo, wewe waaibishe kwa kukaa kimya, endelea kushikilia msalaba maana huo ni uzima wako kama utauachi basi yaliyompata kobe yatakuwa ni Dhahiri kwako.

Yesu alisema atakayevumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka, shikilia Yesu usiachie ukadondoke  JEHANAMU.

Mpendwa msomaji  ninayofuraha kukujulisha kwamba kuanzia jumapili hii tutakuwa hewani tena kupitiaSIBUKA FM.Pia unaweza kuendelea kujifunza kwa njia ya mtandao ikiwamo facebook na watsap kwa namba 0753892961. Uwe na jumapili njema.  .

Advertisements