Panapo majira hayahaya MUNGU atakutoa*
 
Imeandikwa Matendo 12:1 Panapo majira yaleyale herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa.
 
Mpendwa wangu, sio. Herode pekee yake hata kwako wapo watu wenye nia ya kukutenda mabaya sirini au kwa wazi.
 
Napenda tu kukuhakikishia kwamba MUNGU atakutoa iwe kwa siri au waziwazi, tunaona Baada ya kuuawa kwa Yakobo Herode akamkamata na Petro kimyakimya akamtia gerezani ,
 
Namshangaa huyu MUNGU WA KUOKOA Panapo majira yaleyale usiku kimyakimya malaika akamtoa gerezani. Hadi Petro akadhani kuwa anaota ndoto.Yaani MUNGU anafanya mambo mpaka unaweza ukadhania unaota ndoto.
 
Natamka katika Jina la Yesu Panapo majira hayahaya MUNGU akutendee mambo ambayo akili yako haiwezi kuyapima katika Jina kuu la Yesu.Hadi ufikiri kuwa unaota ndoto.
 
Wakikutenda mabaya mbele za watu Mtakatifu wa Israel atakutoa mbele za watu ili wauone utukufu wake.
 
Paulo na Sila walipigwa mbele za watu na MUNGU panapo majira yaleyale akawatoa kwa tetemeko ili wote walioshuhudia aibu yao washuhudie na muujiza wao.
 
Natabiri kwa ajili yako msomaji walioshuhudia aibu yako na watashuhudia ukombozi wako Panapo majira hayahaya katika Jina la Yesu.
 
Paulo akakataa walipotaka kumtoa kwa siri akasema, wametupiga mbele za watu wote nasi hatuwezi kutolewa kwa siri .Matendo 16:37.
Panapo majira hayahaya MUNGU wa mbinguni akutendee mema zidi ya watu wanyoshao mikono kukutenda mabaya .
Andika amina kama unaamini haya!
Ev.Imani Oscar Katana
0753892861
Ikiwa unatamani kusikia mahubiri ya sauti basi jiunganishe nami kwa WhatsApp namba hiyo hapo juu.
pia sikiliza kipindi chetu cha moto ulao kuanzia saa 1 had 2 usiku kupitia SIBUKA FM KILA JUMAPILI.
Advertisements