Mpendwa msomaji utakuwa shahidi jinsi ambavyo wana ndoa wengi  za siku hizi wanavyothamini ajira i kuliko ndoa. Kabla binti hajaoalewa huwa anafunga ndoa kwanza na kazi ndio maana anao uwezo wa kuwaaacha wazazi wake na kuamabatana na kazi lakina hana ujasiri wa kuambatana na mume wake.Hili ni bomu jipya eti wanandoa wameona lakini baada ya harusi hutenganishwa na kilomita nyingi na wanaonana wakati wa likizo. Hebu mpendwa wangu sema mwenyewe hapo pana ndoa au ni uhawala! Kwani ili ndoa iwe ndoa ni lazima ,Mwanzo 2: 24 ichukue nafasi yake” hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”

Hata mbingu zinawashangaa eti mwili mmoja mke yupo mkoa wa naniliuuu na mume mkoa mwingine, hiyo siyo ndoa ya biblia. Kumbuka kila mashine inapotengenezwa hutolewa na kitabu chake ch namna ya kutumia “manual book”. Sasa mtu asipotaka kusoma kijitabu cha maelezo namna yakutumia kifaa basi  aweza kuchukua pasi na akaitumia kuchemshia maji, bila shaka pasi hiyo haitadumu itaharibika upesi.Kadhalika mhasisi wa ndoa MUNGU muumba mbingu na nchi alieleza wazi kwamba mtu atamuacha baba na mama yake ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Kinyume cha hapo ni kutumia pasi kuchemshia maji!

Aisee mwili mmoja halafu mnalala mikoa tofauti, mwili mmoja hulala kitanda kimoja, hula chakula cha aina moja, hutumia bajeti moja. Sasa wewe jiulize hiyo ndoa ya kuwa mbali na mwenzako ni hii aliyoiagiza MUNGU ya mwili mmoja au ipo nyingine. Nawashauri wachungaji wanapofungisha ndoa waulize kwanza kama wana ndoa watakuwa  wanaishi pamoja au mikoa mbalimbali, na kama watajiridhisha kwamba watakuwa mikoa mbalimbali basi wasilitumie kabisa neno hili la mwanzo 2:24 la kusema watakuwa mwili mmoja maana hapo wanalidanganya kanisa kwani watakuwa na ndoa ya miili miwili tofauti.

Tena wanaume nawashauri msijaribu kwenda kwa mkemia kupima D.N.A za watoto kwani mmeyataka wenyewe kujali ajira kuliko ndoa. Maskini Uria Mhiti kutokuambatana na mkwewe kidogo tu kukasababisha mjanja kumdaka 2 Samwel 11:1-27. Na Daudi akamtoa Uria vitani ili aweze kupoteza ushahidi lakini hakuweza. Lakini kwa ndoa za kuishi mbali ni rahisi tu si mkeo anakuambia nilipata mimba kipindi kile nilipokutembelea , kumbe pengine sio. Mwanamke anapaswa kuwa na mumewe kumbuka Hawa alipokuwa peke yake kwa muda kidogo tu tayari akaanguka dhambini, lakini kama Adamu angekuwa yupo karibu Hawa asingelidanganywa na nyoka.

Kumbuka kwamba MUNGU ametaka tuambatane ili tushirikiane, tuwepamoja , tufarijiane, tutiane moyo kama watu wa mwili mmoja. Kwa namna hii ni rahisi kukwepa uzinzi kwani mnakuwa pamoja lakini sasa mke anapokuwa mbali yaweza kuwa sababu ya uasherati na uzinzi kutajwa kwenu. Mungu yamkini alikupa neema ya kuvumilia upweke ulipokuwa kijana, sasa ulipooa ujasiri wako wa kuwa mpweke ulikoma. Sasa unapoendelea kukaa mbali na mwanandoa mwenzio unampa ibilisi nafasi. Wakati maandiko yanasema wazi wala msimpe ibilisi nafasi Efeso 4:27.

Lakini pia wanandoa mnapokuwa pamoja mnalea watoto wenu kwa pamoja, mnawasaidia kufikia hatma zao. Kikawaida  kwa miaka ya nyuma watoto walilewa na mzazi mmoja pale tu wakati mzazi wa pili anapokuwa amefariki. Lakini siku hizi kwa vile watu wanajalia ajira sio tena wanalelewa namzazi mmoja la hasha! Wanalelewa na wadad wa kazi au kwenye vituo maalumu vya kulelea watoto ambapo watoto hukusanywa na mtu mmoja hupewa mshahara wa kuwatunza .Hakika hizi ni nyakati za mwisho upendo wa wengi umepoa.

Narudia  tena hakuna ndoa bila kuambatana, MUNGU hapendezwi na ndoa za aina hii ya kuwa mbalimbali. Ikiwa umeelewa ujumbe  kama kazi yako inakubali kuhama iwe mwanaume au mwanamke jitahidi kuwa karinu na mwenzi wako. Vinginevyo madhara yake ni makubwa

Advertisements