Nakusalimu tena katika jina Takatifu la BWANA wetu YESU KRISTO ninaendelea tena na Makala  hii ya kwa mtini jifunzeni ambapo tunajifunza kwa mifano iliyo hai. Hii ni kusaidia kuelewa mambo ya kiroho kwa urahisi Zaidi Wiki iliyopita nilieleza  kwa habari ya mtu aliyekuwa anamsadia paka kumuokoa  asizame lakini paka akawa namparua,  hakukata tamaa mpaka  alipomuokoa , tukajifunza kwamba kuparuwa kwa paka ndio tabia yake lakini huruma ndio tabia ya mwanadamu, hivyo tusiige tabia ya paka bali tubaki wanadamu wenye huruma na kuendelea kuokoa Maisha ya watu. Karibu katika kisa cha leo…

Palikuwa mtu mmoja ambaye alikuwa na punda wake ambaye amemsaidia siku nyingi  katika kubeba mizigo, Punda huyu alikuwa mzuri  na mtiifu sana kwa bwana wake.siku moja wakati wa jioni giza lilipokuwa linaingia huyu punda alikuwa akipita mwituni kurejea nyumbani, lakini kwa bahati mbaya kumbe kulikuwa na shimo refu limechimbwa eneo lile na huyu punda akawa amedumbukia ndani ya shimo.

Mweye punda akajaribu kujitahidi kumtoa asiweze, Akaomba msaada kwa wana kijiji wenzake wamsaidie nao hawakuweza, mwenye punda akawaambia wana Kijiji wenzake kwamba anajisikia maumivu makubwa moyoni kuondoka na kumuacha punda wake katika lile shimo na akiwa analia kwa kiasi kile, akaomba basi wamsaidie tu kumfukia ikiwa hai ili wasisikie zile kero za kilio cha punda. Basi wakaanza kutupia udongo ndani ya lile shimo na yule punda akawa anaendelea kupiga kelele.

Wakatupa udongo kwa muda mrefu,  kisha wakaona kelele zimetulia wakajua tayari wamemfukia punda na kazikwa akiwa hai na kelele za kilio chake zimekwisha komeshwa. Walipomulika wakamuona punda akiwa hai juu ya ule udongo waliokuwa wakimtupia ili uweze kumzika, wakashangaa kuona yeye amesimama juu yake wakajiuliza imekuwaje?

Kumbe walipokuwa wakirusha udongo juu ya punda alikuwa anautikisa  ule udongo unashuka chini na anakanyaga juui yake, wakati mwingine udongo ulichanganywa na mamwe ukampiga yule punda wala hakujali ailichofanya ni kuutikisa na kuuweka chini ya miguu yake, hivyo akwa anainuka na udongo pamoja na mawe  unabaki chini yeye akawa ananyanyuka na kutahamaki wakatupa udongo na punda akatoka ndani ya shimo akiwa hai, mpendwa msomaji usikubali kuzikwa ukiwa hai.

Maisha tuliyonayo yako mambo mengi yanayotaka kutuzika tukiwa hai, wengine wasipotaka kukuzika kimwili wanataka kuzika kiroho chako na wakati mwingine wanataka kuzika jina lako. Lakini panapo majira hayahaya nimetumwa nikutie moyo , ya kwamba usikubali kuzikwa ukiwa hai.

Watakuja na udongo wa matusi, wakutukane ili ukate tamaa uamue kuachia ngazi, nakusihi katika jina la YESU usikubali kuachia ngazi, na ukazikwa ukiwa hai bali kung’uta matusi yote na kuyaweka chini yakanyage uendelee kuimarika katika Imani, na kuimarika kiroho na kimwili. Kumbuka hili siku zote ni mapanga na malungu tu yanayoweza kukuumiza hata ukavuja damu, maneno  hayana uwezo huo. Inuka jikung’ute usonge mbele ukalitimize kusudi la MUNGU watasema mchana na usiku watalala.

Nakuambia ukweli yule punda kama angelala chini bila kuijikung’uta na kukanyaga udongo ungeweza kufukia, lakini akasimama hakujali mawe yanayodondoshwa kazi ilikuwa ni kuhakikisha vyote vinawekwa chini ya miguuu yake anavikanyaga na  kumsaidia yeye kuinuka.

Huu ndi ukweli kama utakaa kimya nakunyamaza uchumi wako utazikwa kawa macho yako ukiwa unaona, huduma yako itazikwa na mchana kweupe na macho yako yanaona. Komaa usikubali kuzikwa ukiwa hai.

Wajibu wa kuulinda moyo wako ni wako ndiposa andiko hunena, Linda sana moyo wako maana huko ndiko zitokako chemichemi za uzima. Mithali 4:23. Kama usipoulinda moyo wako ufukiwe na huzuni na machungu hata uanze kuona kama Hakuna haja ya kuishi basi uj wa kuhakiisha unajitikisa na kuyakanyaga yote yanayotaka kukuweka chini. HEBU iambie nafsi yako kama Mtunmga Zaburi 42:5 aliyesema  Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.

Usikubali kuzikwa ukiwa hai. Nakutakia baraka kuu za MUNGU tunapouanza mwezi huu was aba ukawe wa baraka kwako. Pia usikose kusikiliza kipindi cha moto ulao kila jumapili saa moja  hadi saa mbili usiku kupitia sibuka fm. Pia waweza kujifunza nami kupitia ukurasa wangu wa Facebook Imani Oscar 

Advertisements