Habari za jumamosi rafiki yangu katika maisha watu huanza vitu vingi lakini hawamalizi.Si jambo jema ni vizuri kupambana kupigana hata dakika ya mwisho bila kukata tamaa.
Mara nyingi watu wanapofanya reference huwa wanawataja wa mataifa mengine lakini, nilifurahi kumsikia mtu wa nchi akifanya reference of inspiration kwa Mtanzania
JOHN STEPHEN AKHWARI
Huyu alikuwa ni mkimbiaji wa kitanzani katika mbio za Marathoni zilizofanyika nchini Mexico 1968 .Ameingia katika vitabu vya dunia kwa sababu ya kupambana hadi mwisho.
katika mbio ndefu za nyika akiwa anakimbia alianguaka na kuteguka mgu na bega, maumivu makali akayapata. Katika wakimbiaji 75 walionza kukuimbia ni wakimbiaji 57 walimaliza mbio wengine waliishia njiani.
Mshindi wa mbio hizo alikuwa Mamo Wolde wa Ethiopia aliyemaliza mbio hizo kwa muda wa 2:20:26 . Mtanzani John hakukubali kukata tamaa pamoja na maumivu makalia akaendelea  kuchechemea na kukimbia  3:25:27 wakati huo zawadi za washindi zimetolewa na jua limeanza kuzama kwa mbali wanamuona Mkimbiaji mmoja akiwa amejaa bandeji akiwa anachechemea , uwanja mzima ukalipuka kumshangilia. Wanahabari wakamfuta na kumuuliza inakuwaje unaendelea kukimbia katika hali hii
My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race.”
AKAWAJIBU NCHI YANGU HAIKUNITUMA KUANZA MILE 5000 , ILINITUMA KUMALIZA MILE HIZI 5000.
Mpendwa  wangu MUNGU hajakuleta Duniani uanze tu, bali anataka umalize safari.
uwe majeruhi au buheri wa afya kamwe usiishie njiani, fuatilia mpaka mwisho tujifunze kwa mtu huyu JOHN STEPHEN AKHWARI.
Wafilip 1:6 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;
MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI
NI MIMI IMANI OSCAR KATANA
0753892961
Advertisements