Mpendwa msomaji wangu ninakusalimu tena katika jina la YESU, ni neema tu ya MUNGU Kuweza kuifikia siku ya leo. Bado ninaendelea na mafundisho yangu ya injili kwa mifano, kama ninavyoyaleta kila jumapili kupitia gazeti la Nyakati ,ninaamini inaendelea kuwa baraka kwako msomaji wangu na unapata nguvu mpya za kuendelea katika ufalme wa MUNGU. Karibu ufuatane nami..

Katika Kijiji kimoja kulikuwa ambacho kilikuwa karibu na mbuga za Wanyama , palikuwa na mfugaji mmoja alaiyekuwa anachunga mifugo yake karibu na mbuga hizo. Siku moja akamuokota mwanasimba akawa analelewa pamoja na kondoo akajifunza kula majani kama kondoo. Akawa na tabia kama ya kondoo  kwani siku zote amezungukwa na kondooo.

Huko mbugani kondoo wakiwaona simba walikuwa wanakimbia, wanapokimbia na mwanasimba akawa anakimbia, siku moja mwana simba akiwa anakunywa maji aliuona uso wake kwenye maji, akawaza akasema , mbona sura yang u inafanana na wale tunaowakimbia.Alipozingatia moyoni mwake akasema sasa wakija sitawakimbia tena.

Na kweli hazikupita siku nyingi simba akaunguruma kondooo wakachanja mbuga, lakini yule mwana simba akasimama huku anatazama na kuona kitakachotokea, wale simba walipofika wakamfurahia na kumkaribisha tena katika ufalme wa simba.

Mpendwa msomaji wakati mwingine umekuwa kama huyu mwana simba ambaye alikuwa anakula majanai na hali ni simba, akajiona kama mwanakondooo kumbe anao uwezo wa kuunguruma na kutiisha, tatizo lako hujajiona uso wako kwamba unafanana na simba wa kabila la Yuda, YESU KRISTO.

Unaposoma Makala hii ninakushauri uanze kujitazama uso wako katika kioo cha neno la MUNGU ndipo utajua yakini kwamba wewe sio paka wewe ni mwana simba wa kabila la Yuda, hupaswi kulia unapaswa kuunguruma katika maombi.

Imeandikwa 1 Peter 2:5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo

Umejiona umechoka , umefulia upo hoi lakini kumbe ukijiangalia uso wako wewe sio paka wewe ni simba , wewe ni uzao wa kifalme , na siku zote mwana wa mfalme anaishi Maisha ya kifalme.kutokana na Maisha unayoyaishi umekata tamaa na kuona kama haiwezekani kwako kutoka, umevunjika moyo leo ninakushauri jambo moja kuu ya kwamba jianngalie uso wako kwemnya kioo cha neno la MUNGU ndipo utajijua wewe ninani.

Mpendwa wangu yule mwana simba alichoka na kuishi Maisha ya kula majani kwa sababu aliishi akitazama mazingira yanayomzunguka kumbe hakupaswa kuyaangalia mazingira alipaswa kujua kwamba yeye sio wa mazingira ya kula majani yeye ni mwana simba. Kamwe usienende kwa kuona bali uenende kwa bali eneda kwa Imani maana imeandikwa  2 Corinthians 5:7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.

Mimi sijui ni jamba gani hilo linalokufanya ujione mdogo, ujione kama hufai na hali imeandikwa ya kwamba yeye alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri mimi nakuambia ukweli kwamba tatizo lako ni moja , bado hujajioona uso wako katika kioo cha neno la Mungu, ukijiona utapata  ujasiri wa kuishi na kurudi katika ufalme .

Ni ninani aliye balozi wa chi yake katika nchi ya ugeni aishiye kimaskini, sikiliza mpendwa balozi wa Marekani anayeishi katika nchi mojawapo ya Dunia ya tatu yaani nchi maskini, kamwe hawezi kuishi kama mmoja kati ya watu hao waishio kimaskini, yeye ataishi kimareakani japo yupo katika nchi maskini . Maana anajua yeye sio wa nchi maskini japo anaishi kwenye nchi maskini.

Ndugu yangu ukweli ni kwamba ukiwa umeokolewa wewe ni balozi wa MUNGU duniani, hivyo unapaswa kuishi sawa nayeye unmayemuwakilisha anavyotaka uishi. Mimi sina uhakika kama uanishi kama yeye alikuumba alivyokupangia uishi. Inuka sasa ujitafakari mimi nakuambia ukae ukijua kwamba wewe sio paka wewe ni simba.

Mpendwa ikiwa unabarikiwa na madhabahu hii, MUNGU akuguse kutoa sadaka yako katika namba iliyoandikwa hapo chini. Pia usiache kusikiliza kipindi chetu cha moto ulao kupitia SIBUKA FM kila siku ya jumapili saa 1 hadi saa 2 usiku. Au karibu katika kundi letu la moto ulao kwa mtandao wa WhatsApp kwa namba 0753892961. Barikiwa jumapili ya leo

Advertisements