Mpendwa msomaji wangu ninakusalimu tena katika jina kuu la YESU KRISTO , karibu tena katika Makala yetu hii ya moto ulao. Nikiendelea kukufundisha kwa mifano ili uweze kuelewa kwa urahisi. Leo  nataka nikueleze  umuhimu wa uchungu katika Maisha…

Mama mjamzito wakati wa kujifungua unapofikia yako maumivu makali anayokabiliana nayo ambayo hujulikana kama uchungu wa uzazi.Utasikia wakiimba nyimbo zote,  na wengine wakiomba MUNGU . utasikia wengine wakitukana waume zao. Hii yote ni kwa sababu tu uchungu umekolea na  daktari mzuri akiona mama hana uchungu basi huongezewa  maji ya uchungu. Kamwe daktari hashughuliki na kutibu uchungu  wa mama mjamzito kwani ucunu usidia mtoto azaliwe.

Hii ni kwa sababu ili uweze kujifungua, au kuzaa mtoto ni lazima upate uchungu, kama kuna maombi ambayo MUNGU hashughuliki nayo kuyajibu basi ni pamoja na kuomba aondoe uchungu wakati wa kuzaa.Nakumbuka mke wangu alinisimulia kwamba alipokuwa anajifungua mtoto wetu wa kwanza alinenena kwa lugha kwa viwango vya juu lakini hata hivyo uchungu haukuondoka na kwa mafanikio akaniletea mtoto wa kiume.

Ndugu yangu mpendwa katika Kristo  yako maumivu ambayo hauna budi kuyapitia ili uweze kufikia mafanikio na ndoto zako. Wapo watu wanapenda asali lakini hawataki kung’atwa na nyuki, labda kwa vile ulikuwa ni msemo wa wahenga kwamba fuata nyuki ule asali , lakini  ni ukweli usiopingika kwamba wakati wowote ili kupata ushindi mkubwa ni lazima kukabiliana na uchungu mkubwa.

Upo mtu unasoma Makala sasa hata saa hii ungali na uchungu mkubwa, lakini sikia sauti ya MUNGU kwamba yeye ni anakuwazia mema,acha kuangalia uchungu, bali utazame uzuri wa mtoto. Mama mja mzito huwa haangalii uchungu bali mtoto kama ilivyoandikwa.

Zab 126:6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.

Mungu anaweza kuruhusu uchungu katika Maisha yako sio kwa sababu anataka kukuangamiza, hasha! Bali kwa sababu anaataka  mambo mazuri yazaliwe katika Maisha yako. Kwa hiyo mtu yeyote makini anapopita kwenye uchungu anajua kuna kitu kizuri kinakwenda kuzaliwa. Ndiposa mtu kama Ayubu utakuta akisema yakuwa  pamoja na uchungu nilionao sasa lakini najua ya kuwa mteteaji wangu yu hai na hatimaye atasimama katika nchi atanitetea. Hata kama mwili wangu utaharibika hivi pasipo mwili huu nitamuona MUNGU Ayubu 19:25-26.

Mtumishi wa Mungu Yakobo anapoandika waraka kwa watu wote anawakumbusha ya kuwa hesabuni kuwa nifurahh kuu mkiangukia katika uchungu, Yakobo 1:2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;Kuangukia kwenye majaribu sio laaana, wal;a sio kuachwa na MUNGU bali ni kama uchungu kwa mama mja mzito unaupitia ili mtoto azaliwe. Unaposoma Makala hii moyo wako uinuke tena usijione kama aliyetupwa na kuteswa na MUNGU bali ujue unaye baba yako mbinguni anayekuwazia mema ili kukupa tumaini katika siku zako za mwisho.

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Yer 29:11 Pamoja na uchungu unaoupitia jambo moja liwe dhahiri kwako ya kwamba YEYE mtakatifu wa Israeli anayajua mawazo anayokuwazia wewe ili kukupa Tumaini katika siku zako za mwisho,endelea kusonga mbele kwani mwisho wa uchungu wako haujafika, utakapofikia basi uwe nauhakiaka ya kwamba mtoto atazaliwa na utasahau uchunggu wako.

Kwani baada ya uchungu mama mja mzito akikumbatia mwana kamwe hakumbuki tena uchungu, bali anaunagalia uzuri wa mtoto.Na wewe piga vizuri hivyo vita vya Imani na mwendo uumalize kisha uipokee taji isiyoharibika mbinguni kwa baba. Ipo taji imeweka utakapomaliza kazi, mimi nakutia moyo  usikatae tamaa, endelea kusukuma mapaka mtoto azaliwe, ukiacha mtoto atafia tumboni . Kumbuka hili siku zote wakati mwin gine Mungu atakupitisha katika maji mengi sio kwa lengo la kukugharikisha ili ufe la hasha, bali unapita kwenye maji mengi ili utoke ukiwa umeogeshwa kwa maji mengi.

Karibu sana kwa group yetu ya WhatsApp  0753892961 ya moto ulao ili uweze kujifunza Zaidi Neno la uzima lakini pia usikose kusikiliza kipindi cha moto ulao leo kuanzia saa moja hadi saa mbili ujifunze Zaidi NENO la MUNGU.

 

Advertisements