Search

Mtumishi Imani Oscar Katana

Category

Be Inspired

KIJANA WA KIUME USIJUTE KWA KUACHWA NA BINTI

MAALUMU KWA VIJANA WA KIUME WALIOUMIZWA NA WACHUMBA/WASICHANA.

KWA VIJANA WA KIUME WENYE MAONO YA KUOA LAKINI BINTI ULIYEMFUTA KAKUTAA BASI JIFARIJI KWA MANENO HAYA.

“A Girl who reject man with vision and follow man with television one day he will watch the man with vision in her husband’s television”
YAANI
“Msichana anayemtosa mwanaume mwenye maono na kumkubali mwanume mwenye magari na television (luninga) siku moja atamuona mwanume aliyemkataa (yule mwenye maono) kwenye television ya Mumewe”
AU
” REJECTION IS DIRECTION” Yaan ‘ kukataliwa ndio njia’ wala kukataliwa sio mateso, maana unapokataliwa unaonyeshwa njia.
najua panauma lakini ndio hivyo, hata kama ni chungu lakini ndio dawa!
Mtoto wa kiume usikonde eti kwa sababu kakumwaga, kawafuta wajanja wa mujini, wewe tulizana na jifariji kwa maneno hayo

******************as the matter of fact,***************
wanaume ndio wachache duniani ukilinganisha na wanawake, mfano katika Tanzania watu wenye sifa za kuoa na kuolewa yaani waliofikisha miaka 18 kwa mujibu wa daftari la kudumu la wapiga kura ni
wanawake 11 950 789
wanaume10 800 589
wanawake 1 149 619 wanazidi.
sasa Rafiki unashindwa hata kufanya kazi , eti umechinjiwa baharini, eti umepigwa kibuti.
JIPE MOYO mdogo wangu MKE WAKO YUPO TU!
Na ukiona anakuchelewesha kutoa jibu, uwe macho ujue pengine anakupima au yupo kwenye uhusiano unaosumbua.
usiwe mzito kufanya maamuzi.

NI USHAURI TU! NI MTAZAMO TU!

NAKUTAKIA USHINDI MDOGO WANGU NA MIMI SIKU MOJA NILIKUWA KAMA WEWE.

NI MIMI KAKA YAKO
IMANI OSCAR KATANA
WhatsApp +225 753 89 29 61.
KARIBU TUJIFUNZE PAMOJA NENO LA MUNGU.

Image may contain: 1 person
Advertisements

NAMNA YA KUPATA KIBALI MBELE ZA MUNGU NA WANADAMU

Mpendwa msomaji wangu naamini upo vyema, karibu sana katika ujumbe wa leo. Mara nyingi watu wamekuwa wakiomba MUNGU awape kibali wakiamini ndio njia pekee ya kupata kibali. lakini nataka kwa mfululizo huu nikufundishe namna unavyoweza kupata kibali mbele za MUNGU na wanadamu karibu fuatana nami!

1.KIBALI HUJA KWA KUTENDA VYEMA.

Mwanzo 4:7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

Hapo tunaona Kaini anachukia na uso wake unakunjamana kwa sababu sadaka ya Habili nduguye imepokelewa na ya kwake haikupokelewa.Akachukia ndipo MUNGU akaamua kumpa siri ya namna ya kupata kibali mpendwa wangu huenda na wewe umekuwa ukikasirika na kuumia kwa vile watu wanapandishwa vyeo kazini na wanapata kibali kwa wengine halafu wewe upo tu. Nakusihi usikasirike na kuukunja uso wako kama Kaini bali jitafakari na uanze kutenda vyema.

Ipo tofauti kati ya kutenda mema na kutenda vyema. Kutenda mema kunahitaji mtu kuzaliwa mara ya pili na kupata nguvu ya kiungu kumsaidia kutenda mema lakini kutenda vyema huja kwa kuwa makini na kupata maarifa ya kufanya kitu kizuri katika eneo fulani.

Hapo ndipo wengi wanapoanza kulalamika mbona waovu wanafanikiwa na mimi kila mara nafunga na kuomba wala sionekani? Sikiliza wenzako wamejifunza kutenda vyema kazini, wanajiongeza na wantumia mbinu zote na hatimaye wanakuzidi kwa kutenda vyema ndipo wao wanapata kibali kwa kutenda mema hata kama sio watenda mema.

Hivyo nakushauri pamoja na kufunga kuomba na kunena kwa lugha lazima ujifunze kutenda vyema ili upate kibali.Unapoomba MUNGU omba akupe ubunifu wa ajabu wa kimawazo na kimatendo ili unapofanya kila mtu aone kwamba hakika wewe ni wa tofauti.Mara zote watu wanoinuliwa ni wale ambao wamekataa kuwa wa kawaida wamejitofautisha Kwa kutenda vyema.

Hebu jitume, ongeza nidhamu na uone kama kibali hakitakujia.

ukitenda vyema utapata kibali.

nakutakia Jumatano njema!

nitaendelea kesho.

Kama ayala anavyoionea shauku mito ya maji ndivyo nafsi yangu inavyokuonea shauku ee MUNGU wangu

haleluya

MUNGU HADHIAKIWI APANDACHO MTU NDICHO ATAKACHOVUNA

The ball full of air can not be immersed in water, it will keep floating.

A PERSON FULL OF HOLYSPIRIT CAN NOT BE DROWNED IN TEMPTETATION OF THIS WORLD WILL KEEP FLOATING IN JESUS MIGHT NAME.

inspire

Blog at WordPress.com.

Up ↑