Search

Mtumishi Imani Oscar Katana

Category

Teachings

HUDUMA NKUHUNGU-DODOMA

MUNGU ni mwema tumekuwa na huduma ya semina, nzuri hapa DODOMA lakini pia tumekuwa live kupitia Maisha FM 100.1. MUNGU NI MWEMA hatutaketi mpaka BWANA afanye imara kanisa lake.

Advertisements

HAKUNA TAJI BILA TIJA

 

Taji ni heshima anayopewa mtu baada ya kufanya kazi kubwa , kwa mfano tunapambana katika ulimwengu huu ili tukapate taji isiyoharibika. Imeandikwa katika kitabu cha 1 Wakorintho 9:25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Mara nyingi tumeimba kwamba tukimaliza kazi tutavalishwa taji, lakini nakukumbusha tu ya kwamba Hakuna taji bila tija.

Ukimuona askari anapigiwan saluti anaheshimiwa basi ujue , huyo amakula mateso kuliko wengine wakati wa mazoezi wala usije ukaona ni suala la bahati . Hapana ujue alisotea kupata manyota ya kutosha watu wanasema amechafuka ,na amejaa nyota katika mwili wake na hii imekuja baada ya mateso  makali na kuyavumilia. Lakini si hivyo tu kuna mambo anayokuwa amefanya yaliyosababisha kumfanya atambuliwe na kutunukiwa heshima hiyo ni Hakuna taji bila tija.

Raisi katika nchi yoyote ya kidemokrasia huwa anaheshimika sana,lakini heshima hii inakuja baada ya kupambana kwenye kampeni na kushinda, utaona wakati wa kampeni anavyotukanwa na kukejeliwa lakini anapoapishwa heshima yake inakuwa haipimiki, anaheshimika na watu wote.

Ndugu yangu mpendwa katika Kristo Hakuna taji bila tija katika jambo lolote, hata katika maswala ya kiroho ukweli uko wazi maandiko yanatufananisha na mkulima mwenye bidii shambani kuwa atavuna Zaidi imeandikwa 2 Wakorintho 9:6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Mungu hadhiakiwi wewe endelea kufurahia wokovu wa YESU , yeye amabaye ni kielelezo cha Imani yetu, alifunga siku arobaini.

Wewe unajiita mtumishi wa MUNGU unawaongoza watu unakula Zaidi kuliko washarika wako, nakukumbusha tu mtumishi yale aliyoyasema mtume Paulo katika kitabu cha 1 Wakorintho 9:27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa. Ndugu yangu natuogope kuwa watu wa kukataliwa , na wewe kama mtumishi wa MUNGU uwe kielelezo kwa waaminio, katika kuutafuta uso wa BWANA. Usiridhike na mafanikio uliyoyafikia bado MUNGU ana mahali pa juu Zaidi anataka kukupeleka na kukuinua endelea kuleta tija katika mwili wa Kristo.

Ndugu yangu nimegundua jambo hili katika utumishi kwamba nguvu ya madhabahu yako inaongezeka kwa kadriambavyo unajitoa kwa BWANA kumtumikia, yaani kuutesa mwili wako na kuutumikisha kwa ajili ya Kristo, kadri unavyozivuna roho nyingi zimjie BWANA ndivyo nguvu zakoa za kiroho na mamlaka yakoa katika ulimwengu war oho ianaongezeka. Lakini pia gharama ya sadaka zinazotolewa katika madhabahu yako, mpendwa katika mambo yote ufahamu tu kwamba lazima ujitoe, uache usingizi kwa ajili ya Kristo.

Mimi mwenzakoa kama uanavyoona jina langu ni mwinjilisti tu wa kawaida, lakini kila siku na kusisitiza kusikiliza kipindi chetu cha radio, tunachokiripia sisi wenyewe kwa pesa za mifukoni mwetu. Kama ujuavyo mtumishi wa MUNGU inachukua muda watu kukufahamu na kujiungamanisha na huduma yako, lakini mpendwa wewe una washarika mia mbili wala hata wilaya yako haikufahamu. Wakati ulipaswa kutumia hiyo redio ya  hapo wilayani kumhubiri Kristo na wilaya yako ikakufahamu na kujua uwepo wako. Yesu alisema anao kondoo walio nje ya zizi , mpendwa injili yako hiyo ni kubwa sio ya kusikilizwa na washarika wako pekee ongeza tija na utapata taji duniani na kisha uzima wa milele , mbinguni.

Hatujaja dunianin kushangaa tumekuja kufanya kazi, maadiko Mhubiri 11:6 Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa,kama ni hii au hii,au kama zote zitafaa sawasawa.Ipo nguvu ya kutumia vyombo vya habari kumhubiri Kristo , tusiwaachie wahuni wawalishe matango pori watanzania, inuka utumie vyombo vya habari kuhubiri injili. Mimi nakukumbusha tu, Hakuna taji bila tija, kama huamini subiri ndani ya miaka mitano ijayo sitakuwa na haja  ya kujitambulisha maana dunia itanijua.

 

MAMBO MATANO YA THAMANI KULIKO PESA ..sehemu ya pili.

Mpendwa msomaji  wiki iliyopita nilianza kukueleza jambo la kwanza ambalo ni muhimu kuliko pesa. Nilieleza jinsi ambavyo jinsi ambavyo jina jema lina thamani kuliko fedha kwa sababu ntu aliyeamua kulinda jina lake hata iwe pesa kiasi gani haiwezi kumbadilisha. Karibu tena siku ya leo

Mara nyingi watu wengi wanadhani ukiwa na pesa basi unakuwa ni mtu mwenye furaha kuliko watu wengine, lakini sikia wakati mwingine mtu anaweza kuwa tajiri ndio lakini pia akawa ndio mwenye huzuni kuliko wote. Wapo watu wanapesa na hawajawahi kupata watu wanaowapenda ila wamezungukwa na watu wanaopenda pesa zao. Waweza kuona mke wa potifa ana mtamani mfanyakazi wa ndani house boy wake.Hii inadhihirisha wazi kwamba hakutoshelezwa na mumewe bali alipenda pesa yake ndio yupo tayari kusaliti ndoa kama Yusufu asingekuwa na hofu ya MUNGU.

Sikiliza pesa sio jibu la mambo yote , inaweza kununua dawa kamwe haiwezi kununua afya na uzima hivyo mtu aweza kuwa na pesa bado akawa ni mtu mwenye afya mbovu.Pesa inaweza kununua nyumba wala haiwezi kununua Amani na furaha ndani ya nyumba.Yapo majumba makubwa na yenye kupendeza lakini ndani yake wanaishi watu wasio na furaha, Imewahi kutokea watu mamilionea wanajinyonga na kuacha ujumbe.Nilikuwa nikisoma kwenye mtandao kuna orodha kubwa ya mamilionea waliojinyonga kwa sababu mbalimbali.

Pesa inaweza kununu nchakula na kikajazwa kwenye majokofu lakini kamwe haiwezi kununua hamu ya chakula. Mtu amejaza vyakula lakini hana hamu ya kula kabisa, lakini wengine kwa sababu ya afya wamekatazwa kula chakula chenye chumvi, sukari , nyama na mapochopocho. Kwa hiyo mtu anabakia anatamani kula chakula kitamu lakini afya yake inamzuia. Wewe unadhani pesa  ni jibu ya mambo yote nakuambia sivyo.

Imeandikwa “ maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.Mhubiri 7:12. Ndio ni kweli pesa ni ulinzi  lakini hekima na maarifa ni bora kuliko fedha. Ni hatari kubwa kwa mtu asiye na hekima kuwa Tajiri au kuwa na pesa kwani upumbbavu wake utazidi.

Kufanikiwa kwa mbumbavu ni kwa maangamizi yake Mithali 1:32b. Mtu akikosa hekima na akapata pesa basi hizo pesa zake zitamwangamiza. Maana kwa jeuri ya pesa aliyonayo atafanya upumbavu ambao mwisho wake utakuwa ni maangamizi yake.

Hekima ni bora kuliko fedha, hekima ni ulinzi, hekima huleta fedha lakini kamwe pesa haiwezi kuleta hekima. Wapo wengi wana pesa lakini hawana hekima, kwani  sio pesa   walizonazo zinazoleta hekima bali hekima na maarifa huja kutokana na MUNGU aliye hai.

Ndugu yangu mpendwa nimekaa nikagundua kwamba pesa  ndio inayoweza kukupa  tabia yako halisi, wapo wengi waliokuwa wakimpenda MUNGU vizuri lakini baada ya kupata pesa wakaona hakuna msaada kwa MUNGU. Huzitegemea pesa zao kama maombi yangehusu kununua gari basi sasa hakuna mamaombi maana uwezo upo. Wengi hujikuta wamezungukwa na majukumu mazito ya kutafuta pesa na hupunguza muda wa mtu kukaa na MUNGU ndio maana wengine walisema , pata pes tujue tabia yako.

Yamkini unyenyekevu, na ucha MUNGU na upole ulio nao ni kwa sababu hauna pesa, pesa hubadilisha tabia za watu. Watu wengi nimekutana nao wameikana Imani ili wapate m kazi, wanadhani pesa huleta utoshelevu . Lakini ujue tu kwamba pesa haiwezi kuleta utoshelevu lakini kumcha MUNGU huleta utoshelevu.

Mpendwa wangu nakusihi umjue, MUNGU maana kumcha MUNGU ni chanzo cha maarifa. Kama unataka kujaaa maarifa basi utafute uso wa MUNGU , kumbuka kwamba sulemani yeye alikuwa na hekima ndiyo aliyoiomba.

Kwa kuwa na hekima Sulemani  anatajwa kuwa alikuwa mtu Tajiri sana kuliko wote, kumbe ni hekima inavuta pesa. Hekima ya ukweli inatoka kwa MUNGU kwani yako mambo mwanadamu ukifanya unajiletea upumbavu kwa mfano, Mhubiri 7:9 Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

Lakini pia Mithali 6:32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.MUNGU akujalie utafute ufalme wake kwa nguvu ujipatie hekima, naye MUNGU atakuzidishia yote unayoyahitaji.Nakutakia baraka jumapili ya leo.

HERI YA SIKU YANGU YA KUZALIWA (HAPPY BIRTHDAY)

Nalikuwa Mtoto nami sasa ni mtu mzima, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula. Zab 37:25

MWINJ: IMANI OSCAR KATANA.

MAMBO MATANO YENYE THAMANI KULIKO FEDHA.

 

Ninayofuraha kukukaribisha katika Makala hii itakayokuwa ya mwenedelezo , yenye kutaja na kuyaelezea mambo yenye thamani kuliko pesa. Karibu fuatana nami…

Ndugu yangu mpendwa pesa imekuwa jambo la muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kiasi kwamba watu wanasema pesa ndio jibu la mambo yote, watu husemka pesa ni sabuni ya roho, na sifa lukuki ambazo pesa imekuwa ikipewa.Pesa huanza kutumiwa hata kabla hujaja duniani  kwani wazazi hutumia pesa kulea mimba, kama wazazi tujuavyo maswaibu ya waja wazito. Kwa pesa watu wamewasaliti wenzao , kwa pesa watu wanauana kisa pesa. Kwa neema ya MUNGU nataka nizungumzie mambo matano yaliyo ya muhimu kuliko pesa.Kila wiki nitazungumzia jambo mojamoja

Imeandikwa katika kitabu cha Mithali sura 22na mstari wa1 “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu.” Jina jema lina thamani kuliko pes heri mtu yule amabaye ameamua kuchagua jina jema kuliko pesa.

Maandiko yanasema wazi kwamba jina jema ni lina thamani kuliko pesa, unapoaamua kuikubali pesa na pesa ikaondoa jina lako tayari pesa imekuwa ya thamani kuliko wewe. Kuna watu wapo kwenye ndoa lakini kwa sababu ya pesa wamekuwa wakiacha wanandoa wenzao na kutoka nje ya ndoa, hapo tayari jina jema la mke au mume limeondoka umepewa jina linguine na shetani  unaitwa mzinzi , Heri mtu yule ambaye analithamini jina lake na kuliona lina thamani kuliko pesa, usiuze utu wako kwa sababu ya pesa. Jina jema lina thamani kubwa kuliko pesa usikubali kupoteza jina jema kwa sababu ya kupenda pesa.

Ukiwa na pesa waweza kuwaburuta watu na wakafanya vile ambavyo unataka, lakini ukiwa na jina jema utaheshimika. Sio kila anayekuita mheshimiwa anakuheshimu, wengine wanaogopa tu nguvu ya pesa uliyonayo.Lakini ukiwa na jina jema utazidi kuheshimiwa kila utakapokuwa.Jina jema huleta kibali na kuheshimika.

Nilisoma kisa kimoja cha baba mmoja ambaye alikuwa ameamua kutaka jina jema, katika utumishi wake alifanya kazi kwa kumuogopa MUNGU. Wengi katika kitengo chake wakawa matajiri lakini sio kwa njia halali walikuwa wanafanaya wizi na kupoeka rushwa. Lakini baba huyu alithamini utumishi wake wa  haki na kutenda kwa haki. Japo alikuwa mkuu hakukubali kuajiri watu kwa rushwa au kutumia cheo chake vibaya.

Miaka ikaenda akastafu, na akawa anaishi Maisha ya kawaida. Siku zake za kuishi duniani zilipokoma akawa anawausia wanawe wamche MUNGU na kumtumikia kwani watabarikiwa. Mmoja kati ya watoto wake akawa anamlaumu na kumuambia baba ulifanya kazi na akina Fulani wote ni matajiri lakini wewe unakufa maskini ni urithi gani unaotuachaia?

Baba yake alimtazama kwa huzuni  wala hakumjibu neno lolote, watoto wake hawakumuelewa. Siku zikaenda na hatimaye yule mzee akafariki. Baada ya kumaliza masomo yake yule mtoto wake mdogo akawa ameomba kazi. Akaitwa kwenye usaili, alishangaa kiongozi wa jopo la usaili akimchangamkia na kumwambia wewe ni mtoto wa mzee Fulani aliyekuwa mwadilifu, kusema kweli yeye ni chanzo cha mimi kuwa hapa. Baada ya usaili yule kijana akahakikishiwa kuipata kazi ile.

Baada ya siku chache akawa amepata kazi na kulipwa mshahara mnono akaheshimiwa na kupendwa kwa sababu ya jina jema alilolijenga baba yake.Ndipo akawa analia kwa uchungu kila akikumbuka maneno aliyokuwa akimlaumu baba yao, kumbe yeye alikuwa amewawekea urithi wa jina jema.

 

Mpendwa msomaji wangu, ni kweli tunapaswa kuwaawekea watoto wetu akiba na urithi, lakini ujue pia kwamba jina jema, na Maisha tunayoyaishi pia waweza  kuwa urithi kwa wanetu.Kwa kadri unavyowatendea wengine unapanda , wekeza katika jina lako kuwa mtu wa maadi wala sio mtu  wa madili na hakika jina jema lina thamani kuu kuliko pesa.

Kamwe katu usikubali kulidhalilisha jina lako kwa ajili ya pesa, pesa hazidumu lakini jina lako litadumu.Kuna watu ni kama bendera hufuata upepo, hawana tabia zao. Tabia zao zinategemea pesa, yaani hata kama alikuwa hataki kufanya jambo Fulani lakini akiambiwa atapewa pesa yuko tayari kuhongwa na kubadili jina lake.

Mungu wa mbinguni akusaidie kulisimamia na kulijali jina lako, jipatie jina jema kuliko pesa na MUNGU hatakuacha uabike, utakuwa mshindi siku zote za Maisha yako. Na bila shaka hutakosa heshima.

 

 

 

UTAUWA PAMOJA NA KURIDHIKA UNA FAIDA KUBWA.

 

Mpendwa msomaji nakusalimu katika Jina kuu la Yesu, ninaamini unaendelea vema na karibu katika Makala ya leo katika kona hii uipendayo ya moto ulao ambapo nitaelezea habari utauwa na kuridhika una faida kubwa. Karibu ufuatane nami..

Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. 1 Tim 6:6 , haya ni maneno ambayo mtume Paulo alikuwa akimuambia kijana wake Timotheo kwa njia ya barua aliyomuandikia  kwamba katika mambo yaliyo na faida maishani basi pia utauwa na kuridhika una faida kubwa.

Kwa habari ya utauwa yaani utakatifu sina haja kuandika kwani kila mtu anajua ya kwamba  ni agizo la MUNGU tuwe watakatifu kama yeye MUNGU alivyo mtakatifu.Wapo wanaopotosha ukwelil kwamba hakuna watakatifu duniani wakati wao wenyewe wanasoma kwamba Mathayo., luka , Marko na Yohana wote ni watakatifu na waliiishi duniani. Nakama hiyo haitoshi imeandikwa katika Zaburi 16:3 ya kuwa watakatifu walioko duniani ndio walio bora ndio ninaopendezwa nao. Mpendwa tunahitaji kuwawatakatifu hili halina mjadala , acha mimi nizungumzie Zaidi leo kwa habari ya kuridhika.

Ndugu yangu mpendwa duniani tunapoishi kuna utofauti mkubwa sana, wako maskini wako matajiri wako wazima  na wako wagonjwa, warefu kwa wafupi, wanene kwa wembamba , vijana kwa wazee, kamwe hatulingani. Mara nyingi moyo wa mwanadamu huwa  ni mdanganyifu nao una ugonjwa wa kufisha ni nani awezaye kuujua Yer 17:9. Watu wamekuwaa na mzigo mzito maishani na wanashindwa kufurahia maisha kwasababu ya kuto kuridhika.

Na  sababu kubwa zakuto kuridhika ni tabia mbaya ya kupenda kujilkinganisha na wengine, watu wengi hawawezi kufurahia Baraka alizowapa MUNGU kwani huwa hawaangalii na kufurahia walichotendewa na BWANA bali huangalia mambo ambayo MUNGGU amewetendea wengine hivyo hujikuta na maumivu na wivu ya kutamani vile ambavyo hawako navyo.

Watu wamejikuta wana roho ya kuto kutosheka, huwa hawatosheki ndio maana mafisadi wala rushwa hawaishi kwani wanaona mishahara yao haitoshi. Wamekaa mkao wa kupiga wanadhani Amani ya mtu ipo  katika wingi wa vitu alivyonnavyo  Luka 12:15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.

Mpendwa msomaji napenda tu kukumbusha kwamba, kutokuridhika huleta manung’uniko na MUNGU huwa anachukizwa sana na Manung’uniko. Ndiposa mtume Paulo anawaandikia Waraka wa kwanza watu Korintho 10:10  Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. Kutokuridhika huleta mauti, wengi wamejikuta na magonjwa ya moyo na matatizo makubwa ni kwasababu hawataki kuridhika.

Lakini mpendwa wangu msomaji, utauwa pamoja na kuridhika una faida kubwa, nakusihi katika jina kuu la YESU upokee moyo wa shukrani na uachane na manung’uniko ili MUNGU aweze kukubariki. Umezuia Baraka za MUNGU kwa sababu ya kutokuridhika kwako, unajikosesha faida na kukukumbusha tu klwa rehema zake MUNGU ya kwamba, utauwa pamoja na kuridhika una faida kubwa.

Mpendwa wangu wewe kwa mfano ukampa mtu kitu, na akaonyesha moyo wa kutokuridhika sijui hata kama utapata moyo wa kuweza kumsaidia wakati mwingine. Ndivyo ilivyo hata kwa MUNGU wetu unakuta amekubarikia kitu, lakini badala ya kushukuru ndio kwanza unatamani kitu cha jirani yako. Ndio  maana MUNGU katika amri zake anakataza mtu kutamani vitu vya jirani yake, YEYE anataka tuwe watu wa kuridhika kwani kuna faida kubwa.

Sikuzote shindana na mafanikio kamwe usishindane na watu kwani kila mtu amaekuja duniani na Baraka zake, wengine tayari wazazi wao wamewawekea misingi. Wengine tayari koo zao zimekwisha kujenga misingi, lakini wengine ndio kwanza tunatoka kwenye blanketi kubwa la umaskini hivyo ni vigumu kujifananisha nawengine. Yohana mbatizaji aliwaambia maaskari waliokuwa wakimuuliza na sisi tufanyaje akawaambia toshekeni na mishahara yenu na msimshitaki mtu kwa uwongo luka 3:14.

Mpendwa msomaji sina nia kukuandikia kwamba uridhike na hali duni, bali ninachotaka kukufundisha ni kutambua kwamba hata sasa MUNGU amekusaidia na kumshukuru hukui ukiendelea kuutafuta uso wake Zaidi ili akujalie kupata Zaidi. Walakini Utauwa pamoja na kuridhika una faida kubwa, barikiwa na uwe na jumapili njema.

 

HATA WAJAPOCHUKIZWA WOTE KWA AJILI YA YESU, MIMI SITACHUKIZWA KAMWEMpendwa msomaji ninakusalimu kwa jina kuu la Yesu Kristo ninaamini umesheherekea vema sikukuu ya pasaka, karibu tuendelee kujifunza tena katika kona hii ya moto ulao.Kipekee ninamshukuru MUNGU sana nimerejea salama kutoka Kyela nilikokuwa naendesha kongamano la Neno la MUNGU wakati wa pasaka. Karibu tuendelee kujifunza…
Kichwa chetu cha somo ni majibu aliyoyatoa Petro akimjibu Bwana wetu Yesu alipowaambia wanafunzi wake kwamba watachukizwa wote kwa ajili yake usiku ule ndipo katika Mathayo26:33 Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kamwe.Pamoja na kuwa kweli Petro alimkana BWANA YESU mara tatu lakini hili jibu limenipa tafakari kubwa, kwani pamoja na kumkana lakini baada ya kujaa roho mtakatifu Petro aliihubiri kweli kwa ujasiri Matendo 2:14. Na waandishi wa karne ya kwanza wanaonesha ya kwamba kusulubishwa kichwa chini miguu juu kwani alisema siwezi kufa kama BWANA YESU, kweli hakuwa tayari kuchukizwa tena.
Mpendwa msomaji wangu ni ukweli usiopingika kwamba kutokana na kuongezeka kwa maasi yapo mengi yanayowafanya watu wachukizwe na Yesu, hawataki tena kusikia mambo ya wokovu wamejitenga na imani wakifuata mafundisho ya mashetani . Lakini kama BWANA WA MAJESHI aishivyo hata wajapochukizwa wote kwa ajili ya YESU wewe na mimi tusichukizwe kamwe!
Watu wamechukizwa na mafundishoya utakatifu, wanaona kana kwamba ni kuwafanya washindwe kwenda na wakati. Ukiwaambia wanawake wavae sawa na mavazi yaipasayo injili ya Kristo na kuwa na mwenendo kama wanawake akina Sara waliowaheshimu waume zao. Utawaona wakizungumzia habari ya usawa wa kijinsia wamechukizwa na maandiko matakatifu na kuyaita yana mfumo dume. Mimi napenda kuwatia moyo mabinti wa Kristo mnaoilinda imani na mseme, Hata wajapochukizwa wote kwa ajili ya Yesu mimi sitachukizwa kamwe!
Zamani watu walihudhuria mikutano ya injili kwa sababu walikuwa wanapenda kuona burudani ya kwaya na nyimbo za injili. Sasa hawana mpango kwani nyimbo na waimbaji waliokuwa wanahitaji kuwaona kwa kuwafuata kwenye mkutano wa injili , wanaweza kuwa na nyimbo zao kwenye simu. Kwa ufupi hivi sasa mambo ya kuburudisha yapo mengi kiasi cha kwamba watu hawana muda wa kutafuta mambo ya mbinguni.Kuna burudani katika simu zao za mikononi, kuna burudani kwenye kompyuta, kna burudani kwenye luninga na ving’amuzi hivyo watu wamebakia kuburudika na hawana muda na na NENO la MUNGU, ndiposa na kukumbusha hata wajapochukizwa kwa ajili ya Yesu, mimi sitachukizwa kwamwe.
Ni nadra sana siku hizi mahala pengi kusikia , injili ya tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia, ni nadrakusikia injili ya kurudi kwa Yesu, ni lini ulipohubiriwa habari za wanawali kumi watanao wapumbavu na watano wenye hekima? Utakuta kwa umri wako ulionao wa miaka hiyo ulijifunza ukiwa kwenye shule ya jumapili ya watoto. Inahubiriwa zaidi habari ya mwanamke mwenye kutokwa damu na kuponywa! Kwenda ulaya, kuwa na pesa na mafanikio kunatajwa zaidi madhabahuni kuliko kukumbushwa kwamba tuko duniani kama wasafiri na wapitaji lakini tunaelekea kwenye mji anaouandaa YESU. Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. 1 Pet 2:11. Hata wajapochukizwa wote kwa ajili yako ee YESU nisaidie mimi na msomaji wangu kamwe tusichukizwe na kweli yako.
Mimi nakukumbusha tu mpendwa msomaji kwamba hizi ni nyakati za mwisho, yawezekana wote katika dhehebu lako wanaweza kuchukizwa na kweli ya MUNGU na wakaanza kujipatia waalimu mafun gu mafungu na kuyafuata mafundisho ya mashetani. 1 Tim 4:1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; Kumbuka hata kama wote wataiacha kweli ya MUNGU na unabii ukatimia kwao wewe ee msomaji wangu , ishike kweli na ujifunge kama mshipi ili Yesu ajapo umlaki mawinguni.
Mimi nimedhamiria, hata wajapochukizwa wote kwa ajili ya YESU mimi sitachukizwa kamwe. Nitaendelea kumwandama BWANA kwa moyo safi hata ajapo nimlaki mawinguni. Barikiwa.

TAARIFA YA HUDUMA YA KYELA

Mpendwa wangu nakusalimu katika jina kuu la YESU!

Napenda kumshukuru MUNGU sana , kwa mkono wake wenye nguvu uliokuwa pamoja nasi katika huduma tuliyoifanya huko KYELA KANISA LA BAPTIST KYELA mjini.

Niliingia mjini KYELA mnamo saa nne usiku nakupokewa na viongozi wa kanisa , kutokea Dar es salaam, kwa bahati mbaya mjomba wangu alifariki siku hiyo. Hata hivyo nilipiga moyo konde kuelekea kwenye huduma na siku ya jumapili tar 9.4.2017 nilianza kwa kuhubiri ibada ya JUMAPILI ambapo kichwa cha somo kilikuwa HATA WAJAPOCHUKIZWA WOT KWA AJILI YAKO, MIMI SITACHUKIZWA KAMWE Math26:33.

SEMINA

Kwa muda wa siku nane nilisimama mufundisha NENO la MUNGU kwa ujasiri wote na mamlaka, yote sawa na alivyoniita. SOMO LA SEMINA LILIKUWA NAMNA YA KUJAA NGUVU ZA MUNGU.Nililifundisha somo hili kwa nguvuna uweza wa ROHO mtakatifu.

MAHUBIRI REDIONI.

Ni maombi yangu Kwa MUNGU kutumia vituo vya Redio kuihubiri injili ya YESU. Hivyo tuliweza kuihubiri injili kila siku nikiwa Kyela kupitia 96.1 Kyela FM inayosikika Nyanda za juu kusini yapata wilaya nane pamoja na nchi jirani ya malawi.Hakika wengi waliisikia NENO la uzima.

UPONYAJI NA KUFUNGULIWA.

Kwa neema ya MUNGU watu wengi waliweza kuponywa kimwili na kiroho.

mtu mmoja aliyekuwa amelazwa hospitali na hawezi kula, aliletwa kwenye chumba cha maombi alipoombewa akafunguliwa, aliporudi nyumbani alitapika kinyama kikiwa ndani ya mfuko wa plastiki.Ambacho inaonekana kiliingia kwa njia ya ushirikina na uchawi baada ya maombi akawa ameweza kuanza kula.

utukufu kwa MUNGU!

 

MBINGU ZINAKUSHANGAA! yaani unathamini ajira kuliko ndoa.?

makala kama ilivyoandikwa gazeti jibu la maisha 26.3.2017
Mpendwa msomaji ninakusalimu katika jina lipitalo majina yote jina la Yesu Kristo wa Nazareti aliyehai karibu tena katika kona hii ya sauti ya mwinjilisti.Napenda kuwashukuru nyote mnaosoma na kunipa mrejesho lakini pia wasomaji wote wa sauti ya mwinjilisti mnaosoma kimyakimya MUNGU na awabariki na mzidi kujitakasa ili Yesu ajapo tukamlaki mawinguni. Sasa fuatana nami katika makala ya leo..
Mpendwa msomaji utakuwa shahidi jinsi ambavyo wana ndoa wengi za siku hizi wanavyothamini ajira i kuliko ndoa. Kabla binti hajaoalewa huwa anafunga ndoa kwanza na kazi ndio maana anao uwezo wa kuwaaacha wazazi wake na kuamabatana na kazi lakina hana ujasiri wa kuambatana na mume wake.Hili ni bomu jipya eti wanandoa wameona lakini baada ya harusi hutenganishwa na kilomita nyingi na wanaonana wakati wa likizo. Hebu mpendwa wangu sema mwenyewe hapo pana ndoa au ni uhawala! Kwani ili ndoa iwe ndoa ni lazima ,Mwanzo 2: 24 ichukue nafasi yake” hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
Hata mbingu zinawashangaa eti mwili mmoja mke yupo mkoa wa naniliuuu na mume mkoa mwingine, hiyo siyo ndoa ya biblia. Kumbuka kila mashine inapotengenezwa hutolewa na kitabu chake ch namna ya kutumia “manual book”. Sasa mtu asipotaka kusoma kijitabu cha maelezo namna yakutumia kifaa basi aweza kuchukua pasi na akaitumia kuchemshia maji, bila shaka pasi hiyo haitadumu itaharibika upesi.Kadhalika mhasisi wa ndoa MUNGU muumba mbingu na nchi alieleza wazi kwamba mtu atamuacha baba na mama yake ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Kinyume cha hapo ni kutumia pasi kuchemshia maji!
Aisee mwili mmoja halafu mnalala mikoa tofauti, mwili mmoja hulala kitanda kimoja, hula chakula cha aina moja, hutumia bajeti moja. Sasa wewe jiulize hiyo ndoa ya kuwa mbali na mwenzako ni hii aliyoiagiza MUNGU ya mwili mmoja au ipo nyingine. Nawashauri wachungaji wanapofungisha ndoa waulize kwanza kama wana ndoa watakuwa wanaishi pamoja au mikoa mbalimbali, na kama watajiridhisha kwamba watakuwa mikoa mbalimbali basi wasilitumie kabisa neno hili la mwanzo 2:24 la kusema watakuwa mwili mmoja maana hapo wanalidanganya kanisa kwani watakuwa na ndoa ya miili miwili tofauti.
Tena wanaume nawashauri msijaribu kwenda kwa mkemia kupima D.N.A za watoto kwani mmeyataka wenyewe kujali ajira kuliko ndoa. Maskini Uria Mhiti kutokuambatana na mkwewe kidogo tu kukasababisha mjanja kumdaka 2 Samwel 11:1-27. Na Daudi akamtoa Uria vitani ili aweze kupoteza ushahidi lakini hakuweza. Lakini kwa ndoa za kuishi mbali ni rahisi tu si mkeo anakuambia nilipata mimba kipindi kile nilipokutembelea , kumbe pengine sio. Mwanamke anapaswa kuwa na mumewe kumbuka Hawa alipokuwa peke yake kwa muda kidogo tu tayari akaanguka dhambini, lakini kama Adamu angekuwa yupo karibu Hawa asingelidanganywa na nyoka.
Kumbuka kwamba MUNGU ametaka tuambatane ili tushirikiane, tuwepamoja , tufarijiane, tutiane moyo kama watu wa mwili mmoja. Kwa namna hii ni rahisi kukwepa uzinzi kwani mnakuwa pamoja lakini sasa mke anapokuwa mbali yaweza kuwa sababu ya uasherati na uzinzi kutajwa kwenu. Mungu yamkini alikupa neema ya kuvumilia upweke ulipokuwa kijana, sasa ulipooa ujasiri wako wa kuwa mpweke ulikoma. Sasa unapoendelea kukaa mbali na mwanandoa mwenzio unampa ibilisi nafasi. Wakati maandiko yanasema wazi wala msimpe ibilisi nafasi Efeso 4:27.
Lakini pia wanandoa mnapokuwa pamoja mnalea watoto wenu kwa pamoja, mnawasaidia kufikia hatma zao. Kikawaida kwa miaka ya nyuma watoto walilewa na mzazi mmoja pale tu wakati mzazi wa pili anapokuwa amefariki. Lakini siku hizi kwa vile watu wanajalia ajira sio tena wanalelewa namzazi mmoja la hasha! Wanalelewa na wadad wa kazi au kwenye vituo maalumu vya kulelea watoto ambapo watoto hukusanywa na mtu mmoja hupewa mshahara wa kuwatunza .Hakika hizi ni nyakati za mwisho upendo wa wengi umepoa.
Narudia tena hakuna ndoa bila kuambatana, MUNGU hapendezwi na ndoa za aina hii ya kuwa mbalimbali. Ikiwa umeelewa ujumbe kama kazi yako inakubali kuhama iwe mwanaume au mwanamke jitahidi kuwa karinu na mwenzi wako. Vinginevyo madhara yake ni makubwa sana baadaye.

Blog at WordPress.com.

Up ↑