Search

Mtumishi Imani Oscar Katana

Category

Testimonies

Atapika nyama iliyovingirishwa kwenye mfuko wa plastiki baada ya maombezi

katika hali isiyo ya kawaida mtu mmoja wilayani Kyela aliyekuwa akiumwa taabaani alitapika nyama, iliyovingirishwa kwenye mfuko wa plastiki baada ya maombezi. Na akawa amepona ugonjwa wake. Baada ya maombezi nilisikia nimepona, lakini baada ya kufika nyumbani nilianza kujisikia kutaka kutapika, nikajaribu kula malimau ili kuituliza hali hiyo lakini sikuweza. Ndipo nikaenda kutapika nikaona mfuko wa plastiki ukiwa umevingirisha kitu ndani yake, nilipojaribu kufungua ndani ndipo nikaona kipande cha nyama, alisema ndugu Bahati ambaye kwa sasa anaendelea vyema baada ya uponyaji. kipande hicho cha nyama ni  kama kinavyoonekana pichani.

Advertisements

Halitasali jiwe juu ya jiwe

Wengi walifunguliwa na kuachwa huru , hapo KYELA watu wenye kifafa walipokea uponyaji na jina kuu la YESU likatukuzwa.

USHUHUDA! Waganga na wachawi hawawezi YESU anaweza.

Ndugu yangu mpendwa nakusalimu katika JINA KUU LA YESU.

Katika kona hii ya shuhuda nataka kumshuhudia MUNGU kwa matendo makuu aliyoyatenda. Pamoja na kuwa mimi ni mhubiri wa injili lakini pia ni Mwalimu wa shule ya sekondari.

nataka kumshukuru MUNGU kwa jinsi ambavyo amekuwa akifanya kwa wanafunzi wangu hapa shuleni ambao wangepaswa kuacha shule kwasababu ya mambo ushirikina. Hebu nikupe shuhuda za wanafunzi wafuatao.

1.Mwanafunzi wa kwanza

Mwanafunzi uyu kwa jina la Asha yeye alikuwa amejiunga  suleni kwetu kidato cha kwanza. Kwa taarifa kutoka kwa wazazi wake Huyu mtoto alisoma  mkoani Tanga na aliweza kushika nafasi ya tatu kiwilaya katika moja ya wilaya za mkoa huo. Alipokuwa nyumbani ghafla mtoto akawa kama kicaa akiongea peke yake na kuto kutaka tena shule kwani alikuwa akumbuki chochote alichowahi kusoma. Wazazi wake wakampeleka Tanga  kupata msaada lakini aikumfaa kitu.

Ndipo nikampigia simu mzazi wake akaniambia mtoto amepagawa na majini na yupo Tanga, nikamwambia anaendeleaja akanijibu ali yake bado sio nzuri ndipo nikamwambia basi mlete alipofika nyumbani kwao Maeneo ya mabibo nikaenda kumuona , niliumia sana kumuona binti yangu wa kidato ca kwanza akiwa katika ali ile akiitika na kusema kama teja.

kwa vile mazinira yaka wa hayaruusu basi tukaja naye mpaka shuleni kwetu DSM BAPTIST maeneo ya Maomeni usalama. Tukaanza maombi baada ya Takribani nusu saa akawa yupo vizuri kabisa akafunguliwa , Tukamruhusu arudi nyumbani, lakini ile ali ikawa inamrudia.

hivyo tukajadiliana na mke wangu  kwamba inabidi akae nyumbani kwangu, tukaanza maombi ilikuwa ni hatari mara atake kuvunja kabati, mara atake kupigga  katoto ketu kadogo lakini tukaendelea kuomba. Yale masetani ndani yake yalikuwa ayataki asome, tukasema lazima asome  KWA JINA LA YESU.

TULIMWITA YESU KWA WIKI MBILI, NA AKAFUNGULIWA KABISA NA HADI SASA YUPO KIDATO CHA NNE ANAENDELEA VIZURI NA MASOMO YAKE. familia yake wana furaha  na Amani

 

HAKIKA TUKIWA NA YESU VIZURI BASI TUNAKUWA CHUMVI YA DUNIA, TUNAONGEZA RADHA DUNIANI NA KATIKA MAISHA YATU.

BWANA YESU ASIFIWE!

Kutibitisha ushuhuda  huu mpigie baba yake mzazi kwa namba 0786197162

KWA MAANA MUNGU WETU NI MOTO ULAO!

MAHOJIANO YANGU NA MJERUMANI

BWANA YESU APEWE SIFA!

Katika majukumu ya kila siku nikiwa kama mkuu wa shule huwa napokea wageni mbalimbali kutoka nchi  mbalimbali. Nikiwa kama mwinjilist natambua kuwa MUNGU ameniweka hapa kwa makusudi kwa ajili ya NENO lake, basi huwa sipotezi muda bali ninawashuhudia NENO la uzima . Safari nilikuwa na mahojiano na Raia mmoja wa Ujerumani kwa jina Nicolaus Jankuhn ilikuwa kama ifuatavyo.

MIMI: Nicolous unaamini kama kuna MUNGU?

NICOLOUS: Siamini kama kuna MUNGU au hakuna MUNGU.

MIMI: haaaa ! lakini unaamini mababu zenu walimuamini MUNGU kiasi cha kuleta dini huku kwetu?

NICOLOUS: Ndio naamini hivyo?

MIMI: Je huoni kwamba MUNGU wa babu zenu, aliwasaidia babu  kwa baraka zake kiasi kwamba ninyi mnafurahia maendeleo hayo.? Na huoni kwamba kuacha kumwabudu nikumkataa na bila shaka mtalaaniwa?

NICOLOUS: Sio kwamba sisi hatumuamini MUNGU , ila hatutaki kwenda kanisani, bali  tunafuata yale babu zetu walifanya kwa kusaidia maskini, kutenda haki  na kuwa mtu mwema.

MIMI: Ahaaa! imeandikwa katika Waebrania 10:25 Wala msiache kukusanyika, kwa hiyo kuacha kwenda kanisani na kusababisha nakanisa kuuzwa ni kwamba mmemuacha MUNGU wa babu zenu. Vipi kuhusu talaka na kukutana kimwili wachumba kabla ya ndoa?

NICOLOUS:Hakuna shida?

MIMI: Sasa sikiliza , ninyi mnafurahia maendeleo makubwa kwa sababu babu zenu, walimwabudu MUNGU wa kweli hivyo ndoa zao zilikuwa imara maana waliifuata biblia inayokataza talaka , Huyo MUNGU  ndiye ambaye sisi huku AFRICA TUNAMWABUDU, KWA HIYO JAMBO JIPYA LITAFANYIKA KAMA ALIVYOWAINUA BABU ZENU WALIPOMWABUDU, ATATUINUA WAAFRICA NA NINYI LAZIMA MTAPOROMOKA TU. MAANA MMEMUASI MUNGU WA KWELI.

NICOLOUS: Anacheka kidogo anasema , inawezekana ikawa kweli lakini sina uhakika!

Ndugu zangu, Ulaya sasa kuna giza kuu, hebu tumtafute MUNGU wa KWELI na tupate nguvu na uweza wa kwenda kuihubiri ulaya itubu.Nitaendelea kumuomba MUNGU mwenye wivu awaonyeshe  hawa watu wa Ulaya kwamba sasa yupo AFRIKA.

MUNGU IBARIKI AFRIKA

MUNGU IBARIKI TANZANIA

KATIKA JINA LA YESU.

 

Blog at WordPress.com.

Up ↑