Search

Mtumishi Imani Oscar Katana

Mambo matano yenye Thamani kuliko Pesa sehemu ya tatu.

Ndugu yangu mpendwa unayefuatilia Makala hii,tayari nimeelezea mambo mawili ambayo yanathamani kubwa kulikom pesa.Nimeeleza habari ya jina jema kwambalina thamani kubwa kuliko pesa, Lakini pia nimeeleza kwamba hekima inathamani kuliko pesa. Leo tunaingia katika jambo la tatu karibu..

Kibali cha MUNGU kina thamni kuliko pesa, mtu mwenye kibali anaweza kununua bila pesa, hapo ndipo utajua maana ya kibali.Wapo watu waliofanya mambo makubwa ukiwauliza sio kwamba walikuwa na pesa nyingi la hasha! Walikuwa na kibali cha MUNGU.

Kibali (favour) ni hali ya kupata upendeleo wa kiungu, yaani popote unapokuwa unaenda MUNGU anakujalia kukubalika na kupendwa watu wanakuwa tayari kukusaidia.Watu wanajitoa Maisha yao kwa ajili yako, popote unapokwenda unajikuta watu wanakufadhili na kukujali.Yusufu alipata kibali kwa potifa na kwa mkuu wa gereza lakini si hivyo tu hata kwa wazazi wake maana mzee Yakobo alikuwa anampedna sana Yusufu. Mwanzo 39:21.

Mtu mwenye kibali cha MUNGU hawezi kubaki chini, namfananisha na mpira uliojazwa upepo ambao hauwezi kuzamishwa kamwe , unaweza ukapiga mbizi nao mpaka chini ya bahari lakini jambo moja nidhahiri utaachiwa na utarudi juu na kuelea.Ndio maana mtu kama Yusufu walimtupa kwenye shimo lakini kibali cha MUNGU kikamtoa shimoni akapelekwa kwa Potifa, Alipotupwa gerezani bado huko na kibali cha MUNGU kikamtoa akajikuta ni miongoni mwa wakuu wan chi ya Misri.

Mpendwa ukiambiwa kukamata vipepeo, kama utaaamua kukimbiza kimoja kimoja na kukamata ni kweli utakamata lakini itakuwa ni kwa taabu sana. Kwani utatumia nguvu nyingi kukamata kwa njia hii lakini njia rahisi ni kupanda bustani ya maua na bila shaka vipepeo watakuja kwenye maua nawe utawakamata kwa urahisi.

Kibali cha MUNGU huvunja mapingo, unaweza ukawa hauna pesa lakini kibali kinakupa kununua bila pesa, tafuta kibali kwa MUNGU ili uweze kuwa na uwezo wa kununua bila pesa.

POTIFA ! YUSUFU SIO WA KUFUNGWA NI WA KUTUZWA. shairi

1.Nakupigia saluti, kamanda mkuu Potifa.

Tena bila shuluti, nina kumwagia sifa.

umevuka vizingiti, huchunguzi taarifa

Yusufu si wa kufungwa, Yusufu ni wa kutuzwa.

 

2. Unamtupaje  jela. akulindiaye heshima.

kijana asiyekera,  ulimjua mapema.

kakataa kula pera, kakulindia heshima.

Yusufu sio wa kufungwa, Yusufu ni wa kutuzwa.

 

3.Jimama limegomewa, kwa aibu linazusha.

Potifa umeambiwa, huna muda kushushu.

kijana ashambliwa, jela unamrusha

Yusufu si wa kufungwa, Yusufu ni wa kutuzwa.

 

4.Pole sana Yusufu, Wema hawana maisha!

Wao wana kukashifu, MUNGU anakusifu.

wewe usiogope bifu,MUNGU ni mkamilifu.

Yusufu si wa kufungwa, Yusufu ni wa kutuzwa!

Shairi hili iwe zawadi kwa wote walio kama Potifa kuhukumu watu bila kufanya uchunguzi wa kina. Pia liwe zawadi kwao waliosingiziwa wajue kwamba MUNGU ATAWATENDEA KAMA ALIVYOFANYA KWA YUSUFU, akamtoa gerzani akawa mkuu katika nchi yote , USIMTENDE DHAMBI ATAKUTENDEA MEMA. mwanzo 39:9

 

 

MAMBO MATANO YA THAMANI KULIKO PESA ..sehemu ya pili.

Mpendwa msomaji  wiki iliyopita nilianza kukueleza jambo la kwanza ambalo ni muhimu kuliko pesa. Nilieleza jinsi ambavyo jinsi ambavyo jina jema lina thamani kuliko fedha kwa sababu ntu aliyeamua kulinda jina lake hata iwe pesa kiasi gani haiwezi kumbadilisha. Karibu tena siku ya leo

Mara nyingi watu wengi wanadhani ukiwa na pesa basi unakuwa ni mtu mwenye furaha kuliko watu wengine, lakini sikia wakati mwingine mtu anaweza kuwa tajiri ndio lakini pia akawa ndio mwenye huzuni kuliko wote. Wapo watu wanapesa na hawajawahi kupata watu wanaowapenda ila wamezungukwa na watu wanaopenda pesa zao. Waweza kuona mke wa potifa ana mtamani mfanyakazi wa ndani house boy wake.Hii inadhihirisha wazi kwamba hakutoshelezwa na mumewe bali alipenda pesa yake ndio yupo tayari kusaliti ndoa kama Yusufu asingekuwa na hofu ya MUNGU.

Sikiliza pesa sio jibu la mambo yote , inaweza kununua dawa kamwe haiwezi kununua afya na uzima hivyo mtu aweza kuwa na pesa bado akawa ni mtu mwenye afya mbovu.Pesa inaweza kununua nyumba wala haiwezi kununua Amani na furaha ndani ya nyumba.Yapo majumba makubwa na yenye kupendeza lakini ndani yake wanaishi watu wasio na furaha, Imewahi kutokea watu mamilionea wanajinyonga na kuacha ujumbe.Nilikuwa nikisoma kwenye mtandao kuna orodha kubwa ya mamilionea waliojinyonga kwa sababu mbalimbali.

Pesa inaweza kununu nchakula na kikajazwa kwenye majokofu lakini kamwe haiwezi kununua hamu ya chakula. Mtu amejaza vyakula lakini hana hamu ya kula kabisa, lakini wengine kwa sababu ya afya wamekatazwa kula chakula chenye chumvi, sukari , nyama na mapochopocho. Kwa hiyo mtu anabakia anatamani kula chakula kitamu lakini afya yake inamzuia. Wewe unadhani pesa  ni jibu ya mambo yote nakuambia sivyo.

Imeandikwa “ maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.Mhubiri 7:12. Ndio ni kweli pesa ni ulinzi  lakini hekima na maarifa ni bora kuliko fedha. Ni hatari kubwa kwa mtu asiye na hekima kuwa Tajiri au kuwa na pesa kwani upumbbavu wake utazidi.

Kufanikiwa kwa mbumbavu ni kwa maangamizi yake Mithali 1:32b. Mtu akikosa hekima na akapata pesa basi hizo pesa zake zitamwangamiza. Maana kwa jeuri ya pesa aliyonayo atafanya upumbavu ambao mwisho wake utakuwa ni maangamizi yake.

Hekima ni bora kuliko fedha, hekima ni ulinzi, hekima huleta fedha lakini kamwe pesa haiwezi kuleta hekima. Wapo wengi wana pesa lakini hawana hekima, kwani  sio pesa   walizonazo zinazoleta hekima bali hekima na maarifa huja kutokana na MUNGU aliye hai.

Ndugu yangu mpendwa nimekaa nikagundua kwamba pesa  ndio inayoweza kukupa  tabia yako halisi, wapo wengi waliokuwa wakimpenda MUNGU vizuri lakini baada ya kupata pesa wakaona hakuna msaada kwa MUNGU. Huzitegemea pesa zao kama maombi yangehusu kununua gari basi sasa hakuna mamaombi maana uwezo upo. Wengi hujikuta wamezungukwa na majukumu mazito ya kutafuta pesa na hupunguza muda wa mtu kukaa na MUNGU ndio maana wengine walisema , pata pes tujue tabia yako.

Yamkini unyenyekevu, na ucha MUNGU na upole ulio nao ni kwa sababu hauna pesa, pesa hubadilisha tabia za watu. Watu wengi nimekutana nao wameikana Imani ili wapate m kazi, wanadhani pesa huleta utoshelevu . Lakini ujue tu kwamba pesa haiwezi kuleta utoshelevu lakini kumcha MUNGU huleta utoshelevu.

Mpendwa wangu nakusihi umjue, MUNGU maana kumcha MUNGU ni chanzo cha maarifa. Kama unataka kujaaa maarifa basi utafute uso wa MUNGU , kumbuka kwamba sulemani yeye alikuwa na hekima ndiyo aliyoiomba.

Kwa kuwa na hekima Sulemani  anatajwa kuwa alikuwa mtu Tajiri sana kuliko wote, kumbe ni hekima inavuta pesa. Hekima ya ukweli inatoka kwa MUNGU kwani yako mambo mwanadamu ukifanya unajiletea upumbavu kwa mfano, Mhubiri 7:9 Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

Lakini pia Mithali 6:32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.MUNGU akujalie utafute ufalme wake kwa nguvu ujipatie hekima, naye MUNGU atakuzidishia yote unayoyahitaji.Nakutakia baraka jumapili ya leo.

HERI YA SIKU YANGU YA KUZALIWA (HAPPY BIRTHDAY)

Nalikuwa Mtoto nami sasa ni mtu mzima, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula. Zab 37:25

MWINJ: IMANI OSCAR KATANA.

MAMBO MATANO YENYE THAMANI KULIKO FEDHA.

 

Ninayofuraha kukukaribisha katika Makala hii itakayokuwa ya mwenedelezo , yenye kutaja na kuyaelezea mambo yenye thamani kuliko pesa. Karibu fuatana nami…

Ndugu yangu mpendwa pesa imekuwa jambo la muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kiasi kwamba watu wanasema pesa ndio jibu la mambo yote, watu husemka pesa ni sabuni ya roho, na sifa lukuki ambazo pesa imekuwa ikipewa.Pesa huanza kutumiwa hata kabla hujaja duniani  kwani wazazi hutumia pesa kulea mimba, kama wazazi tujuavyo maswaibu ya waja wazito. Kwa pesa watu wamewasaliti wenzao , kwa pesa watu wanauana kisa pesa. Kwa neema ya MUNGU nataka nizungumzie mambo matano yaliyo ya muhimu kuliko pesa.Kila wiki nitazungumzia jambo mojamoja

Imeandikwa katika kitabu cha Mithali sura 22na mstari wa1 “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu.” Jina jema lina thamani kuliko pes heri mtu yule amabaye ameamua kuchagua jina jema kuliko pesa.

Maandiko yanasema wazi kwamba jina jema ni lina thamani kuliko pesa, unapoaamua kuikubali pesa na pesa ikaondoa jina lako tayari pesa imekuwa ya thamani kuliko wewe. Kuna watu wapo kwenye ndoa lakini kwa sababu ya pesa wamekuwa wakiacha wanandoa wenzao na kutoka nje ya ndoa, hapo tayari jina jema la mke au mume limeondoka umepewa jina linguine na shetani  unaitwa mzinzi , Heri mtu yule ambaye analithamini jina lake na kuliona lina thamani kuliko pesa, usiuze utu wako kwa sababu ya pesa. Jina jema lina thamani kubwa kuliko pesa usikubali kupoteza jina jema kwa sababu ya kupenda pesa.

Ukiwa na pesa waweza kuwaburuta watu na wakafanya vile ambavyo unataka, lakini ukiwa na jina jema utaheshimika. Sio kila anayekuita mheshimiwa anakuheshimu, wengine wanaogopa tu nguvu ya pesa uliyonayo.Lakini ukiwa na jina jema utazidi kuheshimiwa kila utakapokuwa.Jina jema huleta kibali na kuheshimika.

Nilisoma kisa kimoja cha baba mmoja ambaye alikuwa ameamua kutaka jina jema, katika utumishi wake alifanya kazi kwa kumuogopa MUNGU. Wengi katika kitengo chake wakawa matajiri lakini sio kwa njia halali walikuwa wanafanaya wizi na kupoeka rushwa. Lakini baba huyu alithamini utumishi wake wa  haki na kutenda kwa haki. Japo alikuwa mkuu hakukubali kuajiri watu kwa rushwa au kutumia cheo chake vibaya.

Miaka ikaenda akastafu, na akawa anaishi Maisha ya kawaida. Siku zake za kuishi duniani zilipokoma akawa anawausia wanawe wamche MUNGU na kumtumikia kwani watabarikiwa. Mmoja kati ya watoto wake akawa anamlaumu na kumuambia baba ulifanya kazi na akina Fulani wote ni matajiri lakini wewe unakufa maskini ni urithi gani unaotuachaia?

Baba yake alimtazama kwa huzuni  wala hakumjibu neno lolote, watoto wake hawakumuelewa. Siku zikaenda na hatimaye yule mzee akafariki. Baada ya kumaliza masomo yake yule mtoto wake mdogo akawa ameomba kazi. Akaitwa kwenye usaili, alishangaa kiongozi wa jopo la usaili akimchangamkia na kumwambia wewe ni mtoto wa mzee Fulani aliyekuwa mwadilifu, kusema kweli yeye ni chanzo cha mimi kuwa hapa. Baada ya usaili yule kijana akahakikishiwa kuipata kazi ile.

Baada ya siku chache akawa amepata kazi na kulipwa mshahara mnono akaheshimiwa na kupendwa kwa sababu ya jina jema alilolijenga baba yake.Ndipo akawa analia kwa uchungu kila akikumbuka maneno aliyokuwa akimlaumu baba yao, kumbe yeye alikuwa amewawekea urithi wa jina jema.

 

Mpendwa msomaji wangu, ni kweli tunapaswa kuwaawekea watoto wetu akiba na urithi, lakini ujue pia kwamba jina jema, na Maisha tunayoyaishi pia waweza  kuwa urithi kwa wanetu.Kwa kadri unavyowatendea wengine unapanda , wekeza katika jina lako kuwa mtu wa maadi wala sio mtu  wa madili na hakika jina jema lina thamani kuu kuliko pesa.

Kamwe katu usikubali kulidhalilisha jina lako kwa ajili ya pesa, pesa hazidumu lakini jina lako litadumu.Kuna watu ni kama bendera hufuata upepo, hawana tabia zao. Tabia zao zinategemea pesa, yaani hata kama alikuwa hataki kufanya jambo Fulani lakini akiambiwa atapewa pesa yuko tayari kuhongwa na kubadili jina lake.

Mungu wa mbinguni akusaidie kulisimamia na kulijali jina lako, jipatie jina jema kuliko pesa na MUNGU hatakuacha uabike, utakuwa mshindi siku zote za Maisha yako. Na bila shaka hutakosa heshima.

 

 

 

UTAUWA PAMOJA NA KURIDHIKA UNA FAIDA KUBWA.

 

Mpendwa msomaji nakusalimu katika Jina kuu la Yesu, ninaamini unaendelea vema na karibu katika Makala ya leo katika kona hii uipendayo ya moto ulao ambapo nitaelezea habari utauwa na kuridhika una faida kubwa. Karibu ufuatane nami..

Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. 1 Tim 6:6 , haya ni maneno ambayo mtume Paulo alikuwa akimuambia kijana wake Timotheo kwa njia ya barua aliyomuandikia  kwamba katika mambo yaliyo na faida maishani basi pia utauwa na kuridhika una faida kubwa.

Kwa habari ya utauwa yaani utakatifu sina haja kuandika kwani kila mtu anajua ya kwamba  ni agizo la MUNGU tuwe watakatifu kama yeye MUNGU alivyo mtakatifu.Wapo wanaopotosha ukwelil kwamba hakuna watakatifu duniani wakati wao wenyewe wanasoma kwamba Mathayo., luka , Marko na Yohana wote ni watakatifu na waliiishi duniani. Nakama hiyo haitoshi imeandikwa katika Zaburi 16:3 ya kuwa watakatifu walioko duniani ndio walio bora ndio ninaopendezwa nao. Mpendwa tunahitaji kuwawatakatifu hili halina mjadala , acha mimi nizungumzie Zaidi leo kwa habari ya kuridhika.

Ndugu yangu mpendwa duniani tunapoishi kuna utofauti mkubwa sana, wako maskini wako matajiri wako wazima  na wako wagonjwa, warefu kwa wafupi, wanene kwa wembamba , vijana kwa wazee, kamwe hatulingani. Mara nyingi moyo wa mwanadamu huwa  ni mdanganyifu nao una ugonjwa wa kufisha ni nani awezaye kuujua Yer 17:9. Watu wamekuwaa na mzigo mzito maishani na wanashindwa kufurahia maisha kwasababu ya kuto kuridhika.

Na  sababu kubwa zakuto kuridhika ni tabia mbaya ya kupenda kujilkinganisha na wengine, watu wengi hawawezi kufurahia Baraka alizowapa MUNGU kwani huwa hawaangalii na kufurahia walichotendewa na BWANA bali huangalia mambo ambayo MUNGGU amewetendea wengine hivyo hujikuta na maumivu na wivu ya kutamani vile ambavyo hawako navyo.

Watu wamejikuta wana roho ya kuto kutosheka, huwa hawatosheki ndio maana mafisadi wala rushwa hawaishi kwani wanaona mishahara yao haitoshi. Wamekaa mkao wa kupiga wanadhani Amani ya mtu ipo  katika wingi wa vitu alivyonnavyo  Luka 12:15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.

Mpendwa msomaji napenda tu kukumbusha kwamba, kutokuridhika huleta manung’uniko na MUNGU huwa anachukizwa sana na Manung’uniko. Ndiposa mtume Paulo anawaandikia Waraka wa kwanza watu Korintho 10:10  Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. Kutokuridhika huleta mauti, wengi wamejikuta na magonjwa ya moyo na matatizo makubwa ni kwasababu hawataki kuridhika.

Lakini mpendwa wangu msomaji, utauwa pamoja na kuridhika una faida kubwa, nakusihi katika jina kuu la YESU upokee moyo wa shukrani na uachane na manung’uniko ili MUNGU aweze kukubariki. Umezuia Baraka za MUNGU kwa sababu ya kutokuridhika kwako, unajikosesha faida na kukukumbusha tu klwa rehema zake MUNGU ya kwamba, utauwa pamoja na kuridhika una faida kubwa.

Mpendwa wangu wewe kwa mfano ukampa mtu kitu, na akaonyesha moyo wa kutokuridhika sijui hata kama utapata moyo wa kuweza kumsaidia wakati mwingine. Ndivyo ilivyo hata kwa MUNGU wetu unakuta amekubarikia kitu, lakini badala ya kushukuru ndio kwanza unatamani kitu cha jirani yako. Ndio  maana MUNGU katika amri zake anakataza mtu kutamani vitu vya jirani yake, YEYE anataka tuwe watu wa kuridhika kwani kuna faida kubwa.

Sikuzote shindana na mafanikio kamwe usishindane na watu kwani kila mtu amaekuja duniani na Baraka zake, wengine tayari wazazi wao wamewawekea misingi. Wengine tayari koo zao zimekwisha kujenga misingi, lakini wengine ndio kwanza tunatoka kwenye blanketi kubwa la umaskini hivyo ni vigumu kujifananisha nawengine. Yohana mbatizaji aliwaambia maaskari waliokuwa wakimuuliza na sisi tufanyaje akawaambia toshekeni na mishahara yenu na msimshitaki mtu kwa uwongo luka 3:14.

Mpendwa msomaji sina nia kukuandikia kwamba uridhike na hali duni, bali ninachotaka kukufundisha ni kutambua kwamba hata sasa MUNGU amekusaidia na kumshukuru hukui ukiendelea kuutafuta uso wake Zaidi ili akujalie kupata Zaidi. Walakini Utauwa pamoja na kuridhika una faida kubwa, barikiwa na uwe na jumapili njema.

 

HATA WAJAPOCHUKIZWA WOTE KWA AJILI YA YESU, MIMI SITACHUKIZWA KAMWEMpendwa msomaji ninakusalimu kwa jina kuu la Yesu Kristo ninaamini umesheherekea vema sikukuu ya pasaka, karibu tuendelee kujifunza tena katika kona hii ya moto ulao.Kipekee ninamshukuru MUNGU sana nimerejea salama kutoka Kyela nilikokuwa naendesha kongamano la Neno la MUNGU wakati wa pasaka. Karibu tuendelee kujifunza…
Kichwa chetu cha somo ni majibu aliyoyatoa Petro akimjibu Bwana wetu Yesu alipowaambia wanafunzi wake kwamba watachukizwa wote kwa ajili yake usiku ule ndipo katika Mathayo26:33 Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kamwe.Pamoja na kuwa kweli Petro alimkana BWANA YESU mara tatu lakini hili jibu limenipa tafakari kubwa, kwani pamoja na kumkana lakini baada ya kujaa roho mtakatifu Petro aliihubiri kweli kwa ujasiri Matendo 2:14. Na waandishi wa karne ya kwanza wanaonesha ya kwamba kusulubishwa kichwa chini miguu juu kwani alisema siwezi kufa kama BWANA YESU, kweli hakuwa tayari kuchukizwa tena.
Mpendwa msomaji wangu ni ukweli usiopingika kwamba kutokana na kuongezeka kwa maasi yapo mengi yanayowafanya watu wachukizwe na Yesu, hawataki tena kusikia mambo ya wokovu wamejitenga na imani wakifuata mafundisho ya mashetani . Lakini kama BWANA WA MAJESHI aishivyo hata wajapochukizwa wote kwa ajili ya YESU wewe na mimi tusichukizwe kamwe!
Watu wamechukizwa na mafundishoya utakatifu, wanaona kana kwamba ni kuwafanya washindwe kwenda na wakati. Ukiwaambia wanawake wavae sawa na mavazi yaipasayo injili ya Kristo na kuwa na mwenendo kama wanawake akina Sara waliowaheshimu waume zao. Utawaona wakizungumzia habari ya usawa wa kijinsia wamechukizwa na maandiko matakatifu na kuyaita yana mfumo dume. Mimi napenda kuwatia moyo mabinti wa Kristo mnaoilinda imani na mseme, Hata wajapochukizwa wote kwa ajili ya Yesu mimi sitachukizwa kamwe!
Zamani watu walihudhuria mikutano ya injili kwa sababu walikuwa wanapenda kuona burudani ya kwaya na nyimbo za injili. Sasa hawana mpango kwani nyimbo na waimbaji waliokuwa wanahitaji kuwaona kwa kuwafuata kwenye mkutano wa injili , wanaweza kuwa na nyimbo zao kwenye simu. Kwa ufupi hivi sasa mambo ya kuburudisha yapo mengi kiasi cha kwamba watu hawana muda wa kutafuta mambo ya mbinguni.Kuna burudani katika simu zao za mikononi, kuna burudani kwenye kompyuta, kna burudani kwenye luninga na ving’amuzi hivyo watu wamebakia kuburudika na hawana muda na na NENO la MUNGU, ndiposa na kukumbusha hata wajapochukizwa kwa ajili ya Yesu, mimi sitachukizwa kwamwe.
Ni nadra sana siku hizi mahala pengi kusikia , injili ya tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia, ni nadrakusikia injili ya kurudi kwa Yesu, ni lini ulipohubiriwa habari za wanawali kumi watanao wapumbavu na watano wenye hekima? Utakuta kwa umri wako ulionao wa miaka hiyo ulijifunza ukiwa kwenye shule ya jumapili ya watoto. Inahubiriwa zaidi habari ya mwanamke mwenye kutokwa damu na kuponywa! Kwenda ulaya, kuwa na pesa na mafanikio kunatajwa zaidi madhabahuni kuliko kukumbushwa kwamba tuko duniani kama wasafiri na wapitaji lakini tunaelekea kwenye mji anaouandaa YESU. Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. 1 Pet 2:11. Hata wajapochukizwa wote kwa ajili yako ee YESU nisaidie mimi na msomaji wangu kamwe tusichukizwe na kweli yako.
Mimi nakukumbusha tu mpendwa msomaji kwamba hizi ni nyakati za mwisho, yawezekana wote katika dhehebu lako wanaweza kuchukizwa na kweli ya MUNGU na wakaanza kujipatia waalimu mafun gu mafungu na kuyafuata mafundisho ya mashetani. 1 Tim 4:1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; Kumbuka hata kama wote wataiacha kweli ya MUNGU na unabii ukatimia kwao wewe ee msomaji wangu , ishike kweli na ujifunge kama mshipi ili Yesu ajapo umlaki mawinguni.
Mimi nimedhamiria, hata wajapochukizwa wote kwa ajili ya YESU mimi sitachukizwa kamwe. Nitaendelea kumwandama BWANA kwa moyo safi hata ajapo nimlaki mawinguni. Barikiwa.

Atapika nyama iliyovingirishwa kwenye mfuko wa plastiki baada ya maombezi

katika hali isiyo ya kawaida mtu mmoja wilayani Kyela aliyekuwa akiumwa taabaani alitapika nyama, iliyovingirishwa kwenye mfuko wa plastiki baada ya maombezi. Na akawa amepona ugonjwa wake. Baada ya maombezi nilisikia nimepona, lakini baada ya kufika nyumbani nilianza kujisikia kutaka kutapika, nikajaribu kula malimau ili kuituliza hali hiyo lakini sikuweza. Ndipo nikaenda kutapika nikaona mfuko wa plastiki ukiwa umevingirisha kitu ndani yake, nilipojaribu kufungua ndani ndipo nikaona kipande cha nyama, alisema ndugu Bahati ambaye kwa sasa anaendelea vyema baada ya uponyaji. kipande hicho cha nyama ni  kama kinavyoonekana pichani.

Halitasali jiwe juu ya jiwe

Wengi walifunguliwa na kuachwa huru , hapo KYELA watu wenye kifafa walipokea uponyaji na jina kuu la YESU likatukuzwa.

Blog at WordPress.com.

Up ↑